Loading...

SERIKALI YAFAFANUA KATAZO LA MIFUKO YA PLASTIKI

Loading...
SERIKALI YAFAFANUA KATAZO LA MIFUKO YA PLASTIKI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SERIKALI YAFAFANUA KATAZO LA MIFUKO YA PLASTIKI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SERIKALI YAFAFANUA KATAZO LA MIFUKO YA PLASTIKI
link : SERIKALI YAFAFANUA KATAZO LA MIFUKO YA PLASTIKI

soma pia


SERIKALI YAFAFANUA KATAZO LA MIFUKO YA PLASTIKI

Na Lulu Mussa,Dodoma 

Serikali imejipanga kuhakisha kuwa mifuko mbadala wa plastiki inapatikana kwa wingi ili kukidhi mahitaji. 

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba katika Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika hii leo Jijini Dodoma na kusisitiza kuwa katazo la Mifuko ya Plastiki lililotolewa jana na Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa linakuwa na nguvu kisheria kwa kuandika kanuni za katazo ya mifuko ya plastiki zitakazotangazwa katika gazeti la Serikali chini ya Sheria ya Mazingira na kutoa adhabu kwa kila mtu atakaekiuka utaratibu uliowekwa. 

“Kabla ya Serikali kutangaza hatua ya kupiga marufuku mifuko ya plastiki, ulifanyika utafiti na maandalizi ya mifuko mbadala. Uwezo wa kuzalisha upo na mifuko ya karatasi inayotumika Kenya na Rwanda inatumia malighafi inayozalishwa Mgololo-Iringa,Tanzania.” Makamba alisistiza 

Waziri Makamba ameainisha kuwa kuna vifungashio ambavyo havitapigwa marufuku ambavyo ni pamoja na vifungashio vya dawa za hospitalini, vifungashio katika sekta ya kilimo na ujenzi pia vile vya kuhifadhi maziwa na kutolea mfano wa vifungashio vya maziwa ya ASAS na Tanga Fresh, hata hivyo utaratibu maalumu utawekwa kwa wamiliki wa kukusanya vifungashio hivyo mara baada ya matumizi yake. 

Akizungumzia juu ya ushirikishwaji, Waziri Makamba amesema kuwa zoezi hili limekuwa ni shirikishi na hatua iliyotangazwa na Waziri Mkuu sio ya kushtukiza kwa kuwa Ofisi yake iliratibu mikutano katika maeneo kadhaa nchini kusikiliza maoni ya wananchi kuhusu zuio la mifuko ya plastiki. 

Katika kukamilisha utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu, Waziri Makamba amesema Ofisi yake imeunda kikosi kazi cha kusimamia katazo hilo kikihusisha wajumbe kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira, Mamlaka ya Mapato Tanzania, Idara ya Uhamiaji, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, Shirika la Viwango Tanzania, Mamlaka ya Chakula na Dawa, Jeshi la Polisi na Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali. Wengine ni Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 

Katika hatua nyingine Waziri Makamba amesema kuwa mapema wiki ijayo ataitisha mkutano wa wawekezaji wa mifuko mbadala kote nchini na kujadili kwa kina namna bora ya kuwekeza katika uzalishaji wa mifuko mbadala rafiki wa mazingira. 

Serikali imetangaza kuanzia Juni Mosi 2019 kuwa ni marufuku kutengeneza, kuingiza, kuuza na kutumia mifuko ya plastiki kwa ajili ya kubebea bidhaa za aina yoyote na matumizi yake.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akiongea na waandishi wa Habari kufafanua tamko la Serikali la kupiga marufuku uzalishaji, usambazaji na matumizi ya mifuko ya plastiki hapa nchini. Mkutano huo umefanyika hii leo katika jengo la PSSSF jijjini Dodoma.


Hivyo makala SERIKALI YAFAFANUA KATAZO LA MIFUKO YA PLASTIKI

yaani makala yote SERIKALI YAFAFANUA KATAZO LA MIFUKO YA PLASTIKI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI YAFAFANUA KATAZO LA MIFUKO YA PLASTIKI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/04/serikali-yafafanua-katazo-la-mifuko-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "SERIKALI YAFAFANUA KATAZO LA MIFUKO YA PLASTIKI"

Post a Comment

Loading...