Loading...
title : SIMBA KUIVAA TP MAZEMBE APRILI 6 MWAKA HUU
link : SIMBA KUIVAA TP MAZEMBE APRILI 6 MWAKA HUU
SIMBA KUIVAA TP MAZEMBE APRILI 6 MWAKA HUU
Na Agness Francis, blogu ya Jamii.
ZIMEBAKI siku 4 wawakilishi wa Tanzania klabu bingwa barani Afrika Simba SC kuwavaa TP Mazembe ya nchini Congo katika mchezo wa robo fainali.
Mchezo huo utakaoanza kutimua vumbi majira ya saa kumi jioni Aprili 6 mwaka huu katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salam kwa viingilio vya 4000 mzunguko, VIP B 10000, VIP A 20000, huku tiketi za platinum zikiuzwa kwa 100,000, na mchezo wa marudiano kati ya timu hizo utafanyika April 12 2019 mjini Lubumbashi huko nchini Congo.
Msemaji wa Simba SC Haji Manara akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, amesema kuwa kuelekea mchezo huo
kauli mbiu yao ya Yes we can ndio itakayotumika tena dhidi ya mchezo huo, ambapo pia ilitumika kwenye hatua ya makundi dhidi ya JS Saoura na Allyahal ambapo walifanikiwa kupata matokeo mazuri wakiwa katika uwanja wa nyumbani.

Hata hivyo Msemaji huyo amekanusha uvumi unaozagaa kuhusu mgomo wa Nyota wao tegemezi Emmanuel Okwi raia wa Uganda pamoja na Cloutous Chama kutoka nchini.
"Sio kweli kuhusu taarifa zinazozagaa kuhusu kugoma kwa wachezaji wetu hao, walipata ruhusa ya mwalimu na sasa wamesharejea kambini kuendelea na mazoezi pamoja na wenzao" amesema Manara.
Manara amemalizia kwa kusema kuwa "hakuna mchezaji kutoka Afrika Mashariki anayeweza kugoma kuchezea Simba, tumepoke maombi mengi kutoka kwa wachezaji wa ndani na nje ya nchi kwa barua ili tuwasajili na wengine wanaotoka klabu kubwa tu hapa nchini kila mtu anataka kuchezea Simba.
Hivyo makala SIMBA KUIVAA TP MAZEMBE APRILI 6 MWAKA HUU
yaani makala yote SIMBA KUIVAA TP MAZEMBE APRILI 6 MWAKA HUU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SIMBA KUIVAA TP MAZEMBE APRILI 6 MWAKA HUU mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/04/simba-kuivaa-tp-mazembe-aprili-6-mwaka.html
0 Response to "SIMBA KUIVAA TP MAZEMBE APRILI 6 MWAKA HUU"
Post a Comment