Loading...
title : VANESSA MDEE MIKONONI MWA CHEGE... KISA NJEGEKA
link : VANESSA MDEE MIKONONI MWA CHEGE... KISA NJEGEKA
VANESSA MDEE MIKONONI MWA CHEGE... KISA NJEGEKA
Na Khadija Seif,Globu ya jamii
NYOTA wa muziki kizazi kipya a.k.a Bongo Fleva Said Juma a.k.a Chege amewapa zawadi mashabiki wake kwa kuipua wimbo mpya unaokwenda kwa jina la Njegeka ambayo amemshirikisha Vanessa Mdee.
Akipiga stori ya Michuzi Blog jijini Dar es Salaam Chege amesema kibao hicho ambacho tayari kina video yake amesema ameamu kumshirikisha Mdee ili kuleta ladha hasa kwa kuzingatia ni mwanadada mwenye kipaji cha hali ya juu katika muziki.
"Nimekuwa nikitamani kufanya kazi na Vanessa Mdee zaidi ya miaka mitatu iliyopita lakini sasa nimefanikiwa kumshirikisha kwenye wimbo wangu mpya.Vanesa ni msanii wa kipekee na tofauti kutokana na kujitoa kwake kwenye ngoma pale anaposhirikishwa, kushauri ,ikiwezekana hata kuongeza baadhi ya vionjo na kuifanya kazi ikapendwa,"amesema.
Ameongeza mashabiki wataona ngoma yake Njegeka ilivyokuwa tofauti na ya kipekee na kwamba Njegeka maana yake ni mapenzi yasioeleweka yani ya kudanganyana.
Akizungumzia Meneja anayemsimamia kwenye shughuli zake za muziki, Chege amesema bado yupo kwenye mikono ya Meneja Said Fella lakini kwa sasa kutokana na majukumu ya kijamii inamlazimu asionekane nae kwenye mizunguko yake katika kazi za sanaa.
Wakati huo huo amesema kuwa mitandao ya kijamii ni sehemu kubwa ya kufahamiana na mashabiki wake kwani amekuwa akijifunza mengi na kujua mashabiki wake wanahitaji nini kutoka kwake.
Hivyo makala VANESSA MDEE MIKONONI MWA CHEGE... KISA NJEGEKA
yaani makala yote VANESSA MDEE MIKONONI MWA CHEGE... KISA NJEGEKA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala VANESSA MDEE MIKONONI MWA CHEGE... KISA NJEGEKA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/04/vanessa-mdee-mikononi-mwa-chege-kisa.html
0 Response to "VANESSA MDEE MIKONONI MWA CHEGE... KISA NJEGEKA"
Post a Comment