Loading...

VIJANA WAASWA KUJISHUGHULISHA NA UJASIRIAMALI ILI KUJIAJIRI

Loading...
VIJANA WAASWA KUJISHUGHULISHA NA UJASIRIAMALI ILI KUJIAJIRI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa VIJANA WAASWA KUJISHUGHULISHA NA UJASIRIAMALI ILI KUJIAJIRI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : VIJANA WAASWA KUJISHUGHULISHA NA UJASIRIAMALI ILI KUJIAJIRI
link : VIJANA WAASWA KUJISHUGHULISHA NA UJASIRIAMALI ILI KUJIAJIRI

soma pia


VIJANA WAASWA KUJISHUGHULISHA NA UJASIRIAMALI ILI KUJIAJIRI


Na Woinde Shizza Michuzi TV, Arusha

Tatizo la ajira kwa Vijana ni changamoto kubwa nchini na ulimwengu mzima kwa ujumla, hivyo Vijana wametakiwa kujishughulisha na shughuli za ujasiriamali zenye heshima na staha.

Hayo yamebainishwa katika mahafali sita ya kidato cha sita ya shule ya
Sekondari St. Mary’s Duluti hayo yamebainishwa na Father Fr.Peter Makao alipokuwa mgeni rasmi wa mahafali ya sita katika shule hiyo ambapo alisema katika ulimwengu wa sasa ajira ni chache sana ukilinganisha na idadi ya watu wanaoingia katika soko la ajira.

Alibainisha kuwa ushindani katika soko la ajira ni kubwa sana hivyo ni vyema Vijana wengi waliopo majumbani na mitaani kuliko kukaa bila kazi yeyote ile wakajihusisha na shughuli za ujasilia mali zenye heshima na staha, pia wawe wabunifu

Aliongeza kuwa Vijana walio wengi wa leo wanapenda kuwa huru(freedom) katika kufanya mambo ,Uhuru si jambo baya lakini uhuru usiokuwa na mipaka na uwajibikaji huo sio uhuru,Lazima mtu awajibike kwa matendo yake mwenyewe Hivyo basi uhuru wa kweli lazima uendane na uajibikaji

Akiongea katika mahafali hayo mkuu Wa shule hiyo brother Essau Mlengule aliwaambia kuwa hatua waliofikia ni kwa sababu ya bidii kubwa, nidhamu na kujituma katika masomo mbali na hivyo pia kumtegemea Mwenyezi Mungu, akazibariki nguvu na bidii zao katika kuyatekeleza majukumu yao mema.

Aliwataka wakaendelee kujituma, kuwa na bidii na nidhamu pindi tu warudipo nyumbani pia wasiache hata siku moja kumtegemea Mungu katika kilajambo walifanyalo

Alisema kuwa kuhitimu kwao kwa masomo ni ishara ya kuwa wamekomaa kiakili, kiroho na kimwili na wapotayari kuelekea hatua mpya ya maisha kitaaluma, na maisha ya kujitegemea kiujumla.

"Ninyi kama wasomi wa kidato cha sita, mnajukumu kubwa la kuwa wachangiaji wakubwa katika maendeleo ya maisha yenu binafsi, maendeleo ya familia, jumuniya zenu na hatimaye maendeleo ya Taifa zima la Tanzania kwa fikra yakinifu, kwa matendo na kwa njia halali zinazokubalika na jamii ya watu walioelimika." Alisema Mlengule

Alisema kwamba mafanikio/maendeleo ya kweli hayaji kwa njia za mkato, kutokufuata taratibu za jumuiya husika, Kujichukulia maamzi bila ruhusa ya mamlaka husika, bali kwa kufanya kazi kwa bidii na kwa malengo, kujiamini, kuwa weledi (kuwa wabobezi) katika kazi zenu, elimu ya fedha pamoja na kuwa na nidhamu ya fedha.

Alisema Elimu yenu ya kidato cha sita iwasaidie kuwa na ujasiri wa kuishi kwa mifano maisha ya uadilifu katika familia na jumuiya pia Elimu mliopata iwasaidie kuepukana na uvivu, ulevi, uzushi, kiburi, wizi, matumizi ya madawa ya kulevya, uasherati na matendo mengine maovu yasiyokubaalika katika jamii yetu ya Tanzania kwani jamii inatarajia kuona ndani yenu maisha ya fadhila, utulivu, usikivu, uwajibikaji, ushiriki wenu katika kazi za kiuchumi na kijamii

Alitaja baadhi ya changamoto zinazokabili shule hiyo ni pamoja na upungufu Wa mabweni ,ukosefu Wa jengo la utawala pamoja na viwanja vya michezo.



Hivyo makala VIJANA WAASWA KUJISHUGHULISHA NA UJASIRIAMALI ILI KUJIAJIRI

yaani makala yote VIJANA WAASWA KUJISHUGHULISHA NA UJASIRIAMALI ILI KUJIAJIRI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala VIJANA WAASWA KUJISHUGHULISHA NA UJASIRIAMALI ILI KUJIAJIRI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/04/vijana-waaswa-kujishughulisha-na.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "VIJANA WAASWA KUJISHUGHULISHA NA UJASIRIAMALI ILI KUJIAJIRI"

Post a Comment

Loading...