Loading...

Matapeli waanza kuharibu taswira ya Tanzanite

Loading...
Matapeli waanza kuharibu taswira ya Tanzanite - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Matapeli waanza kuharibu taswira ya Tanzanite, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Matapeli waanza kuharibu taswira ya Tanzanite
link : Matapeli waanza kuharibu taswira ya Tanzanite

soma pia


Matapeli waanza kuharibu taswira ya Tanzanite


Wankyo Gati, Arusha

BAADHI ya wauzaji wa madini ya Tanzanite mkoani Arusha, wamelalamikia uwepo wa madini bandia ya Tanzanite hali ambayo imekuwa ikikwamisha soko la madini hayo.

Akizungumza na gazeti hili mmoja wa wahanga wa utapeli huo Gidion Lekasho alisema kuwa yeye alinunua madini bandia ya Tanzanite ya Sh. milioni 8.

Alisema kutokana na matukio hayo kuendelea kila siku sasa ni wakati muafaka kwa wizara ya madini kulifuatilia suala hilo hasa katika maonyesho ya madini ya vito yanayotarajiwa kufanyika hivi karibuni.

“Katika kipindi cha hivi karibuni kumekuwepo na tatizo la uwepo wa madini bandia ya Tanzanite hali mbayo inatajwa kutishia soko la madini hayo, huku baadhi ya wauzaji wakipata hasara,” alisema.

Mjiolojia  kutoka  Wizara ya Nishati na Madini Kanda ya Kaskazini, Salome Timanywa alisema madini yanapochimbwa yana umbo lake, hivyo wao kama wataalamu wanatambua kutokana na umbo la madini hayo.

Alisema wamejipanga vizuri ili waweze kukabiliana na hiyo changamoto na kuwataka wauzaji kufika wizarani ili kuweza kubaini madini feki na ambayo siyo feki.

Kaimu Kamishna wa Madini Kanda ya Kaskazini, Adam Jumaa alikiri kuwepo kwa tatizo hilo la madini bandia na kueleza kuwa katika maonyesho ya madini ya vito yatakayofanyika, tayari wana wataalamu wa kuyatambua madini hayo.


Hivyo makala Matapeli waanza kuharibu taswira ya Tanzanite

yaani makala yote Matapeli waanza kuharibu taswira ya Tanzanite Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Matapeli waanza kuharibu taswira ya Tanzanite mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/04/matapeli-waanza-kuharibu-taswira-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Matapeli waanza kuharibu taswira ya Tanzanite"

Post a Comment

Loading...