Loading...

NI LAZIMA JAMII KWA UJUMLA WAKE IUNGANE KUPIGA VITA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA

Loading...
NI LAZIMA JAMII KWA UJUMLA WAKE IUNGANE KUPIGA VITA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa NI LAZIMA JAMII KWA UJUMLA WAKE IUNGANE KUPIGA VITA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : NI LAZIMA JAMII KWA UJUMLA WAKE IUNGANE KUPIGA VITA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA
link : NI LAZIMA JAMII KWA UJUMLA WAKE IUNGANE KUPIGA VITA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA

soma pia


NI LAZIMA JAMII KWA UJUMLA WAKE IUNGANE KUPIGA VITA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA

Vita dhidi ya matumizi ya madawa ya kulevya ni vita ngumu na inayopaswa kushirikishwa kwa jamii nzima na ulazima wa ushiriki wa kila mtu kibinafsi na umoja wetu lengo likiwa ni kutokomeza kabisa biashara hii haramu ya madawa ya kulevya ili kuokoa nguvu kazi inayopotea kwa kasi ziadi sababu ya madawa hayo. Vijana ndio waathirika wakubwa wa tatizo hili kwani ni tatizo linaloendelea kukua miongoni mwa vijana na lisipochukuliwa hatua za haraka na maksudi litafifisha ustawi wa jamii ikiwemo kuangamiza kabisa ustawi wa kizazi kijacho. Kwa miaka ya karibuni tumeaona jinsi wasanii wenye majina makubwa wakipotelea katika janga hilo na kuacha kabisa kufanya kazi yao ambayo ingeweza kuwapatia kipato kizuri kwao na familia zao na taifa kunufaika kupitia kazi zao. Mifano ya kina TID, Chid Benz nk ni miongoni mwa vijana wengi wanaohitaji msaada wa jamii kutoka katika dimbwi hili.

Mhe. Paul Makonda, RC Dar es salaam

Mwezi jana kijana shupavu na jasiri Mhe. Paul Makonda ambaye ni mkuu wa mkoa wa Dar es salaam aliamua kulivalia njuga janga hili na kujitoa muhanga kupambana na walanguzi wa madawa haya ili kuokoa vijana wa mkoa wake wasiendelee kuingia katika tatizo hili. Vita hii iliyoanzia kwa Makonda ilisambaa katika mikoa yote Tanzania kiasi cha kusikia kila pembe ya Tanzania ama watuhumiwa wakikamatwa au kuteketezwa kwa dawa hizo. Juhudi za Makonda ziliweza kufukua hadi sheria ya kupambana na madawa ya kulevya na kuweza kuundwa tume itakayoshughulikia vita hiyo. Licha ya vita ya Makonda ilikuwa na mapungufu kadhaa kimbinu ila ilikuja wakati sahihi na badala ya kumshambulia jamii ilipaswa kumpongeza kwa uthubutu aliouonesha na tuungane nae kwa umoja wetu tukishirikiana na Tume iliyoundwa kupambana vita kunusuru kizazi hichi na kijacho.

Leo nimekuletea madhara ya aina mojawapo ya madawa ya kulevya aina ya HEROINE. Tunaposema madawa ya kulevya ni hatari ni vyema hili likaeleweka kwa watanzania wote. Hatari ya Heroine na Madawa mengine ya kulevya ni kubwa sana kwa kizazi hiki na nguvu kazi ya taifa letu na dunia nzima.

Heroine hustua seli za ubongo kuzalisha homoni aina ya Dopamine ambayo humfanya mtu kusikia raha. Homoni hii hutolewa kwa kiasi cha unit 1200- 1800 baada ya kutumia heroine kulinganisha na unit 150 - 200 tu zitolewazo wakati mtu anaposhiriki ngono. Ndio kusema Heroin inaleta raha karibu mara tisa ya ile itokanayo na ngono, tena kwa muda wa takribani dakika 30-40. Raha hii huitwa kwa kitaalamu Euphoria.

Homoni hizi za dopamini hutolewa kwa wingi sana kiasi cha kuufanya mwili kutengeneza vipokezi (receptors) zaidi na zaidi. kwa hiyo mwili hutamani heroin zaidi na zaidi ili kukidhi matakwa ya vipokezi vinavyozalishwa. Hali hii huishia kumfanya mtumiaji kuhitaji idadi kubwa zaidi ya heroin (tolerance).

Arosto (withdraw symptoms); Wakati Heroin inapoisha mwilini, mwili hutamani zaidi. Hapo ndipo hutokea arosto, ambapo  mtumiaji hutaabika kwa kukosa raha isiyo kifani. Maumivu makali ya tumbo, viungo na kichwa, baridi kali, mapigo ya moyo kwenda kasi, mwili kutetemeka, kujisikia vibaya sana, kuchoka, kushindwa kula na dalili nyingine mbaya humpata. Hali hiyo humlazimu kwa haraka sana kutafuta namna ya kuipata Heroin iwe kwa njia halali au haramu. Mwisho inawageuza watumiaji kuwa mazezeta(teja).

Vita hii ya madawa ya kulevya inapaswa kupiganwa na wote bila kuangalia utofauti wa itikadi za kisiasa au malengo ya makundi.



Hivyo makala NI LAZIMA JAMII KWA UJUMLA WAKE IUNGANE KUPIGA VITA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA

yaani makala yote NI LAZIMA JAMII KWA UJUMLA WAKE IUNGANE KUPIGA VITA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala NI LAZIMA JAMII KWA UJUMLA WAKE IUNGANE KUPIGA VITA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/04/ni-lazima-jamii-kwa-ujumla-wake-iungane.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "NI LAZIMA JAMII KWA UJUMLA WAKE IUNGANE KUPIGA VITA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA"

Post a Comment

Loading...