Loading...

STORI UHAKIKI WA VIBALI VYA UKAAZI KWA KUTUMIA MFUMO WA KIELEKTRONIKI

Loading...
STORI UHAKIKI WA VIBALI VYA UKAAZI KWA KUTUMIA MFUMO WA KIELEKTRONIKI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa STORI UHAKIKI WA VIBALI VYA UKAAZI KWA KUTUMIA MFUMO WA KIELEKTRONIKI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : STORI UHAKIKI WA VIBALI VYA UKAAZI KWA KUTUMIA MFUMO WA KIELEKTRONIKI
link : STORI UHAKIKI WA VIBALI VYA UKAAZI KWA KUTUMIA MFUMO WA KIELEKTRONIKI

soma pia


STORI UHAKIKI WA VIBALI VYA UKAAZI KWA KUTUMIA MFUMO WA KIELEKTRONIKI

mwambawahabari
Displaying Pix 01b.jpg

Kamishna Jenerali  wa Idara ya Uhamiaji Dkt. Anna Makakala akifafanua jambo kwa  waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa mfumo mpya wa kielektroniki wa uhakiki  vibali vya ukaazi ujulikanao kama  “E – Verification” mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Displaying Pix 02.jpg
Kamishna Jenerali  wa Idara ya Uhamiaji Dkt. Anna Makakala (kulia) akizungumza na maafisa Uhamiaji na  waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa mfumo mpya wa kielektroniki wa uhakiki vibali vya ukaazi ujulikanao kama  “E – Verification” mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Displaying Pix 03.jpg
Baadhi ya maafisa Uhamiaji na waandishi wa habari wakimsikiliza Kamishna Jenerali  wa Idara ya Uhamiaji Dkt. Anna Makakala (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa mfumo mpya wa kielektroniki wa uhakiki  vibali vya ukaazi ujulikanao kama  “E – Verification” mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Displaying Pix 04.jpg

Displaying Pix 04b.jpg
Kamishna Jenerali  wa Idara ya Uhamiaji Dkt. Anna Makakala (kulia) akifuatilia jambo wakati wa uzinduzi wa mfumo mpya wa kielektroniki wa uhakiki vibali vya ukaazi ujulikanao kama  “E – Verification” mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Afisa Utawala na Fedha wa Uhamiaji Edward Chegero na kushoto ni Afisa wa vibali na Pasi wa Uhamiaji Musanga Etimba.
Picha zote na Eliphace Marwa - Maelezo


Frank Mvungi-Maelezo
Serikali imezindua mfumo wa Kielektroniki wa Uhakiki  wa Vibali vya ukazi “e-verification” hapa nchini ili kuongeza tija na kudhibiti upotevu wa mapato.
Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa mfumo huo.
Akizungumzia mfumo huo Kamishna Jenerali Makakala amesema utasaidia Makampuni,Taasisi,  Mashirika na watu binafsi kuhakiki vibali vya watumishi wao ili kuona kama ni halali ama  si halali na idara hiyo itakuwa tayari kuwasaidia wale wote watakaokuwa na matatizo kupata ufumbuzi wa changamoto zao.
“Idara inatoa siku 90 kwa watu wote kuhakiki vibali vyao vya ukazi ili kama wana matatizo wasaidiwe kupata ufumbuzi” Alisisitiza Dkt Makakala.
Akizungumzia lengo la mfumo huo Makalala amesema utasaidia kuimarisha udhibiti wa wageni wanaoishi hapa nchini na kuzuia mianya ya upotevu wa maduhuli ya Serikali na mfumo huo ni rahisi na unatoa fursa kwa wageni wote wenye vibali vya ukaazi kuhakikiki kumbukumbu za vibali vyao ili kujua kama vimetolewa na Idara hiyo.
Aidha,Idara ya Uhamiaji inawaomba wadau wa huduma zake kufika wao wenyewe katika Ofisi zao katika  ngazi ya Wilaya, Mikoa na Makao Makuu kwani huduma za Uhamiaji hazina uwakala.

Mfumo huo wa uhakiki wa vibali vya ukaazi kwa kutumia njia ya kielektroniki “e-verification” unapatikana kupitia tovuti ya uhamiaji ya http://ift.tt/1R3Brey.




Hivyo makala STORI UHAKIKI WA VIBALI VYA UKAAZI KWA KUTUMIA MFUMO WA KIELEKTRONIKI

yaani makala yote STORI UHAKIKI WA VIBALI VYA UKAAZI KWA KUTUMIA MFUMO WA KIELEKTRONIKI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala STORI UHAKIKI WA VIBALI VYA UKAAZI KWA KUTUMIA MFUMO WA KIELEKTRONIKI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/04/stori-uhakiki-wa-vibali-vya-ukaazi-kwa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "STORI UHAKIKI WA VIBALI VYA UKAAZI KWA KUTUMIA MFUMO WA KIELEKTRONIKI"

Post a Comment

Loading...