Loading...

TRA Yaja na Mikakati Mipya Ya Ukusanyaji Kodi

Loading...
TRA Yaja na Mikakati Mipya Ya Ukusanyaji Kodi - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TRA Yaja na Mikakati Mipya Ya Ukusanyaji Kodi, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TRA Yaja na Mikakati Mipya Ya Ukusanyaji Kodi
link : TRA Yaja na Mikakati Mipya Ya Ukusanyaji Kodi

soma pia


TRA Yaja na Mikakati Mipya Ya Ukusanyaji Kodi


Na Husna Saidi na Nuru Juma- MAELEZO

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekusanya Trilioni 10.87 mpaka kufikia Machi mwaka huu kwa mwaka wa fedha 2016/2017.

Hayo yamesemwa na Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo Charles Edward Kichere wakati wa mahojiano na mtangazaji wa TBC1 Rashid Salum katika kipindi cha Tunatekeleza kinachorushwa kila siku za Jumatatu saa moja kamili jioni na Alhamisi saa tatu na nusu usiku.

Kichere alisema, mwaka huu wa fedha 2016/2017 TRA inatakiwa kukusanya Trilioni 15.105 na hadi kufikia Machi mwaka huu TRA imefanikiwa kukusanya Shilingi Trilioni 10.87.

Aliendelea kwa kusema kuwa mpaka kufikia Juni mwaka huu TRA itahakikisha inatimiza lengo la kukusanya Shilingi Trilioni 15.105 ili kusaidia Serikali kuleta maendeleo kwa wananchi wake.

Alisema kuwa TRA ina waajiriwa wapya ambao wamepewa mafuzo ya miezi sita katika chuo cha kodi juu ya mifumo mbalimbali ya ukusanyaji kodi ambao waliajiriwa moja kwa moja na mamlaka hiyo kwaajili ya kutekeleza majukumu ya ukusanyaji kodi ndani ya nchi.

“Tunatumia mfumo wa Tehama kukusanya kodi na mifumo mingine mbalimbasli kama vile Tigo Pesa , Airtel Money na MPesa ili kurahisishia watu kulipa kodi wakiwa nyumbani na kuepuka usumbufu,” alisema Kichere.

Kichere aliongeza kuwa kwa mwaka huu wa fedha mapato yameongezeka mpaka kufikia asilimia 9.9 hadi 10 licha ya kuwa kuna baadhi ya maeneo hawakuweza kukusanya.

Aidha Kichere alisema Mamlaka kwa sasa imejipanga kuwa na mahusiano mazuri na wafanyabiashara ili kuhakikisha wafanyabiashara wanalipa kodi stahiki na kwa mujibu wa sheria bila kutumia nguvu au uonevu wowote.

Hata hivyo mamlaka hiyo imekuwa ikitoa elimu kwa walipa kodi kwa kupitia vyombo mbalimbali vya habari, kutoa semina kwa watumishi wa umma , kuandaa makongamano ambayo yanatoa elimu, kupitia mitandao ya kijamii na ziara mbalimbali ambazo wamekuwa wakizifanya ili kuhakikisha wafanyabiashara wanapata elimu pamoja na kujua wajibu wao katika kulipa kodi ili kuleat maendeleo nchini.


Hivyo makala TRA Yaja na Mikakati Mipya Ya Ukusanyaji Kodi

yaani makala yote TRA Yaja na Mikakati Mipya Ya Ukusanyaji Kodi Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TRA Yaja na Mikakati Mipya Ya Ukusanyaji Kodi mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/04/tra-yaja-na-mikakati-mipya-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "TRA Yaja na Mikakati Mipya Ya Ukusanyaji Kodi"

Post a Comment

Loading...