Loading...
title : Wananchi Gongolamboto walilia daraja
link : Wananchi Gongolamboto walilia daraja
Wananchi Gongolamboto walilia daraja
Dotto Mwaibale
MANISPAA ya Ilala imeombwa kufanya jitihada za makusudi kunusuru daraja linalounganisha Gongolamboto na Machinjio ya Pugu kwani liko hatarini kusombwa na maji.
Mwito huo ulitolewa Dar es Salaam jana na wakazi wa Pugu Machinjioni wakisema hatua za haraka zisipochukuliwa mawasiliano ya wananchi wa Gongolamboto yatakatika na kuwa adha kwao.
"Tunaomba Manispaa ilifanyie ukarabati daraja hili ambalo kwa sehemu kubwa kingo zake zimesombwa na maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha," alisema Omari Mshamu mkazi wa eneo hilo.
Mkazi mwingine Marietha Stanslaus alisema iwapo daraja hilo litasombwa na maji watakaopata shida zaidi ni wanafunzi watakaolazimika kutumia njia ndefu kufika shuleni kwa kuwa wengi wao wanasoma shule za Gongolamboto.
Jithada za kumpata Diwani wa eneo hilo kuzungumzia suala hilo zilishindikana baada ya simu yake kutopatikana.
Hivyo makala Wananchi Gongolamboto walilia daraja
yaani makala yote Wananchi Gongolamboto walilia daraja Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Wananchi Gongolamboto walilia daraja mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/04/wananchi-gongolamboto-walilia-daraja.html
0 Response to "Wananchi Gongolamboto walilia daraja"
Post a Comment