Loading...

Shekhe aomba vita vya mihadarati viendelee

Loading...
Shekhe aomba vita vya mihadarati viendelee - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Shekhe aomba vita vya mihadarati viendelee, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Shekhe aomba vita vya mihadarati viendelee
link : Shekhe aomba vita vya mihadarati viendelee

soma pia


Shekhe aomba vita vya mihadarati viendelee


Hussein Ndubikile

Mussa Shabani
SHEKHE wa Mkoa wa Dodoma, Mussa Shabani, ameiomba Serikali kuendeleza vita dhidi ya dawa za kulevya ili kudhibiti mmomonyoko wa maadili katika jamii na upotevu wa nguvukazi ya Taifa.

Alitoa mwito huo akiwa Dar es Salaam baada ya kumalizika kwa kongamano la mmomonyoko wa maadili na athari za dawa za kulevya lililoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Kupambana na Kudhibiti Dawa za Kulevya.

Alisema vita hivyo havipaswi kukoma na badala yake Serikali iwachukulie hatua za kisheria watakaoibainika kujihusisha na matumizi na biashara hiyo, huku akisisitiza viongozi wa dini kutoa mafundisho kwa waamini wao dhidi ya athari ya dawa hizo.

"Tuhakikishe kila mtu anakuwa mlinzi ndani ya familia na jirani zake tusiachie Serikali pekee, kwani vita hivyo ni jukumu la kila mmoja wetu," alisema Shekhe Shabani.

Alisisitiza kuwa endapo jamii itashuhudia watu wanaotumia na kuendesha biashara ya dawa za kulevya wanachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria za nchi kasi ya vitendo hivyo viovu itapungua.

Aliongeza kuwa asilimia kubwa ya vijana ndio walioathiriwa na dawa hizo hali inayochangia mmonyoko wa maadili na kutaka wazazi kuwaangalia kwa umakini ili kuwaepusha wasijiingize kwenye utumiaji na uuzaji dawa hizo.

Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Bakwata Taifa, Shekhe Hamis Mataka alisema Baraza litaendelea na programu ya umuhimu wa kupambana na dawa hizo itakayoanzia ngazi ya Msikiti katani, wilayani hadi mkoani.

Shekhe Mataka alisema Bakwata itazindua kitabu kitakachoitwa Kiongozi kikiwa na mafundisho ya kujenga jamii kimaadili na kupambana na dawa za kulevya.





Hivyo makala Shekhe aomba vita vya mihadarati viendelee

yaani makala yote Shekhe aomba vita vya mihadarati viendelee Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Shekhe aomba vita vya mihadarati viendelee mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/04/shekhe-aomba-vita-vya-mihadarati.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Shekhe aomba vita vya mihadarati viendelee"

Post a Comment

Loading...