Loading...

Jaji Mkuu asifu kasi kesi Mahakama za Mwanzo

Loading...
Jaji Mkuu asifu kasi kesi Mahakama za Mwanzo - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Jaji Mkuu asifu kasi kesi Mahakama za Mwanzo, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Jaji Mkuu asifu kasi kesi Mahakama za Mwanzo
link : Jaji Mkuu asifu kasi kesi Mahakama za Mwanzo

soma pia


Jaji Mkuu asifu kasi kesi Mahakama za Mwanzo

Mary Gwera, Mahakama

Profesa Ibrahim Khamis Juma
KAIMU Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Khamis Juma, amesifu kasi ya uondoshaji wa mashauri katika ngazi za mahakama za mwanzo na wilaya.

Alisema hayo jana katika ukumbi wa mikutano ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Manyara alipokuwa akizungumza na watumishi wa mahakama mkoani 

Alikuwa katika ziara yake ya kwanza tangu kuteuliwa kwenye nafsi hiyo Januari, mwaka huu.

Prof. Juma alisema kuwa wananchi wengi bado wana imani na mahakama hizo, hivyo idadi kubwa ya mashauri yameendelea kufunguliwa katika mahakama nchini hususani za chini

“Takwimu tulizo nazo kwa mwaka jana, asilimia 71 ya mashauri yalifunguliwa katika Mahakama za Mwanzo, 14 Mahakama ya Wilaya, asilimia saba, mahakama za hakimu mkaz, asilimia tano Mahakama Kuu na asilimia 0.5 mahakama za rufani,” alieleza.

Aliendelea kusema kuwa takwimu hizo zinaonesha dhahiri kuwa wananchi bado wana imani kubwa na mahakama nchini na hivyo kuwataka mahakimu na watumishi wote wa mahakama kuongeza bidii katika kuwatumikia wananchi.

Mbali na pongezi hizo, aliwataka watumishi hao kufanya kazi kwa kuzingatia mpango mkakati wa mahakama.

“Wengi wenu mnafahamu kwa sasa, mahakama ipo katika utekelezaji wa mpango mkakati wake wa miaka mitano, wenye lengo la kuboresha maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuboresha huduma ya utoaji haki nchini pamoja na kurejesha imani ya wananchi kwa chombo chao,” alisema.

Aliwataka kujikita katika Matumizi ya TEHAMA ili kurahisisha utendaji kazi huku akitilia mkazo kwa Watumishi pia kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya kazi.

Awali, akisoma hotuba yake mbele ya Jaji Mkuu, Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mahakama ya Hakimu Mkazi Manyara, Mhe. Devotha Kamuzora alisema kuwa Mahakama katika mkoa huo zimekuwa zikifanya kazi ya uondoshaji mashauri kwa jitihada ili kuhakikisha kuwa inaondokana na mlundikano wa kesi.

“Kwa upande wetu, mahakama kanda ya Manyara tumejiwekea mkakati wa kuhakikisha kuwa kesi yoyote inayoletwa katika mahakama ya mwanzo, wilaya isizidi miezi mitatu mpaka kukamilishwa kwake na hili tunalisimamia kuhakikisha tunaondokana na mlundikano wa mashauri katika Mahakama zetu,” alisema Kamuzora.

Ziara ya Kaimu Jaji Mkuu imelenga katika kuangalia utendaji kazi wa Mahakama hizo, mafanikio na changamoto wanazokabiliana nazo na hatimaye kushughulikia changamoto hizo kwa ustawi wa Mahakama.



Hivyo makala Jaji Mkuu asifu kasi kesi Mahakama za Mwanzo

yaani makala yote Jaji Mkuu asifu kasi kesi Mahakama za Mwanzo Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Jaji Mkuu asifu kasi kesi Mahakama za Mwanzo mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/05/jaji-mkuu-asifu-kasi-kesi-mahakama-za.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Jaji Mkuu asifu kasi kesi Mahakama za Mwanzo"

Post a Comment

Loading...