Loading...

JICA yatoa bilioni 36/- za maji

Loading...
JICA yatoa bilioni 36/- za maji - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa JICA yatoa bilioni 36/- za maji, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : JICA yatoa bilioni 36/- za maji
link : JICA yatoa bilioni 36/- za maji

soma pia


JICA yatoa bilioni 36/- za maji


Mary Mtuka

SHIRIKA la Maendeleo la Kimataifa la Japani (JICA) limetoa msaada wenye thamani Sh bilioni 36 katika kuendeleza sekta ya maji mkoani Tabora.

Taarifa iliyotolewa jana na Mwakilishi Mkuu wa JICA nchini, Toshio Nagase amesema msaada huo utaongeza wigo wa usambazaji maji safi na salama vijijini mkoani humo.

"Ni mara ya kwanza nchini mradi mmoja kufanikiwa kuchimba jumla ya visima virefu 115 katika eneo kame kama Tabora ambao hali yake ya kihadrolojia si rafiki kupata maji safi na salama," alisema.

Alisema mradi huo utanufaisha watu zaidi ya 40,000 ambao watapata maji safi na salama kwenye vijiji kusudiwa ikiwa ni ongezeko la asilimia 30 kutoka asilimia 9.9 ya mwaka 2009.

Nagase alisema Shirika hilo lilipokea maombi ya kuchimba visima na kufanya utafiti wa awali kuanzia mwaka 2009 hadi 2011 ambapo uchimbaji rasmi ulikamilika mwaka jana.

Aidha, alisema mwanzoni mradi huo ulipata changamoto kama za ugumu wa kupata vyanzo sahihi vya maji safi na salama.

Alisema mradi huo ulihusisha ufungaji pampu za mikono na ujenzi wa miradi minne ya kusambaza maji na ujenzi wa sehemu za umma za kuchotea maji.

Mwakilishi huyo alisema mbali na ujenzi wa miundombinu ya maji, mradi huu pia umesaidia mkoa na wilaya kuanzisha na kusajili vyama vya kijamii (COWSOs) kwa ajili ya kusimamia uendeshaji na matengenezo ya miundombinu ya maji iliyokamilika.


Hivyo makala JICA yatoa bilioni 36/- za maji

yaani makala yote JICA yatoa bilioni 36/- za maji Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala JICA yatoa bilioni 36/- za maji mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/05/jica-yatoa-bilioni-36-za-maji.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "JICA yatoa bilioni 36/- za maji"

Post a Comment

Loading...