Loading...

Serikali yahojiwa utayari kukabiliana na ujambazi

Loading...
Serikali yahojiwa utayari kukabiliana na ujambazi - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Serikali yahojiwa utayari kukabiliana na ujambazi, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Serikali yahojiwa utayari kukabiliana na ujambazi
link : Serikali yahojiwa utayari kukabiliana na ujambazi

soma pia


Serikali yahojiwa utayari kukabiliana na ujambazi


Mwandishi Wetu

Esther Bulaya
MBUNGE wa Bunda Mjini, Esther Bulaya (Chadema) ameitaka Serikali kueleza ilivyojipanga kukabiliana na ujambazi mkoani Mara licha ya kujitokeza katika maeneo mengi nchini.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni alisema Serikali inatambua kuwa hivi karibuni kumeibuka wimbi la matukio ya kihalifu hivyo si kwa mkoa huo tu, bali kila eneo.

Alikuwa akijibu swali la Bulaya bungeni jana ambapo alisema katika kukabiliana na hayo, Jeshi la Polisi nchini limeendelea kubuni mikakati kadhaa na linafanya uchambuzi wa mwenendo wa matukio hayo na kuwapa mbinu askari ya kuja na mikakati.

Alisema hatua nyingine ni kutabiri matukio ya uhalifu kwa kutumia takwimu na mabadiliko ili kutambua wahusika, wanakoishi na namna ya kukabiliana nao.

Aliongeza kuwa wamejipanga kutambua maeneo ambayo yamekuwa yakitumika kama vituo vya uhalifu na kufanya msako kwa doria, kuimarisha ulinzi nchini na kuchukua hatua kali kwa wahusika wanapobainika.

Katika swali la nyongeza Bulaya alisema kufanya doria ni jambo zuri lakini haliwezi kufanyika bila magari mazuri na ya kutosha akihoji mkakati wa Serikali kutoa gari jipya ili kusaidia doria.

Masauni alisema alilichukua swali hilo kama changamoto na kwamba magari yakipatikana mkoa huo utakuwa wa kwanza kupewa ili kuwezesha askari kwenye doria.

Aidha, alisema kuwa eneo la Tunduma mkoani Mbeya, nalo ni changamoto kwa uhalifu, kwa kuwa liko mpakani hivyo watahakikisha nalo linachukuliwa hatua mapema.


Hivyo makala Serikali yahojiwa utayari kukabiliana na ujambazi

yaani makala yote Serikali yahojiwa utayari kukabiliana na ujambazi Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Serikali yahojiwa utayari kukabiliana na ujambazi mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/05/serikali-yahojiwa-utayari-kukabiliana.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Serikali yahojiwa utayari kukabiliana na ujambazi"

Post a Comment

Loading...