Loading...
title : Maalim Seif ‘amchongea’ Lipumba kwa Gwajima
link : Maalim Seif ‘amchongea’ Lipumba kwa Gwajima
Maalim Seif ‘amchongea’ Lipumba kwa Gwajima
Celina Mathew
Maalim Seif Sharif Hamad |
KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad ameutua mgogoro wa chama che kwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima huku kiongozi huyo wa kidini akitangaza kuwa atamlipua Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba Jumapili ijayo.
Akizungumza Dar es Salaam jana wakati alipomtembelea Askofu Gwajima, Maalim Seif alibainisha kwamba amemweleza kiongozi huyo mambo mbalimbali ikiwemo suala la mgogoro ndani ya CUF, aliodai umesababishwa na Lipumba.
Alisema kuwa ameamua kwenda kwa Askofu Gwajima kumweleza hayo kwa sababu ni rafiki yake na hawajaonana siku nyingi lakini pia kiongozi huyo alikuwa haelewi mgogoro wa CUF umesababishwa na nani.
"Nimemweleza Askofu Gwajima mambo mengi hususani mgogoro wa CUF hivyo ataamua mwenyewe nini afanye kutokana na niliyomweleza,"alisema.
Aliongeza kuwa mbali na kwenda kwa Gwajima pia ameshazungumza na viongozi wengine wa dini husuani ya Kiislamu.
Kwa upande wake, Askofu Gwajima alisema kuwa ameshafahamu chanzo cha mgogoro huo kwa kuwa Maalim ni rafiki yake wa siku nyingi lakini Lipumba hana urafiki naye.
Alipoulizwa kama watu watarajie chochote kutokea kuhusu CUF, Maalim Seif na Lipumba kwenye ibada Jumapili ijayo, Gwajima alijibu: “Kumbe mnajua, subirini Jumapili ifike nitamlipua na tutajua amekula maharage ya wapi.”
Hivyo makala Maalim Seif ‘amchongea’ Lipumba kwa Gwajima
yaani makala yote Maalim Seif ‘amchongea’ Lipumba kwa Gwajima Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Maalim Seif ‘amchongea’ Lipumba kwa Gwajima mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/05/maalim-seif-amchongea-lipumba-kwa.html
0 Response to "Maalim Seif ‘amchongea’ Lipumba kwa Gwajima"
Post a Comment