Loading...
title : MADIWANI WAPONGEZA UONGOZI WA HALMASHAURI YA ARUSHA KWA HATI SAFI YA UKAGUZI
link : MADIWANI WAPONGEZA UONGOZI WA HALMASHAURI YA ARUSHA KWA HATI SAFI YA UKAGUZI
MADIWANI WAPONGEZA UONGOZI WA HALMASHAURI YA ARUSHA KWA HATI SAFI YA UKAGUZI
Na: Elinipa Lupembe
Wajumbe wa baraza la madiwani halmashauri ya Arusha wameupongeza uongozi wa halmashauri hiyo kuwezesha kupata hati safi kufuatia ripoti ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali kwa mwaka wa fedha 2015/2016.
Baraza la madiwani |
Munguabela Kakulima, mweka hazina halmashauri ya Arusha |
"Mheshimiwa Mwenyekiti napenda kulitaarifu baraza lako tukufu kuwa halmashauri yetu imapata hati safi kwa mara ya tatu mfululizo " alisema Kakulima.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Arusha, Mheshimiwa Noah Lembris ametoa pongezi kwa uongozi wa halmashauri pamoja na wadau wa maendeleo kwa ushirikiano wao uliopelekea kupata hati safi.
"Nitoe pongezi zangu za dhati kwa mkurugenzi, Idara ya Fedha, watumishi wote, wadau wa maendeleo pamoja na wajumbe wa baraza hili la madiwani kwa pamoja wamesababisha upatikanaji wa hati safi " alisema Mwenyekiti.
Hata hivyo Mheshimiwa Lembris amewataka watumishi wa halmashauri kufanyakazi kwa uadilifu kwa kusimamia kanuni, taratibu na miongozo mbalimbali ya usimamizi na matumizi ya fedha ili halmashauri iendelee kupata hati safi hata kwa mwaka huu tena.
Hata hivyo Mweka hazina huyo alisema kuwa upatikanaji wa hati safi unategemea zaidi matumizi yanayozingatia kanuni, taratibu na sheria pamoja na ushauri kutoka kwa wataalamu wa ndani na nje ya halmashauri hasa wajumbe wa kamati ya ukaguzi.
Halmashauri ya Arusha imepata hati safi kufuatia ripoti ya mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali iiyowasilishwa na mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali Prof. Mussa Jumma Assad aliyoiwasilisha kwa mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Sehemu ya hati ya ukaguzi wa hesabu za serikali,
Hivyo makala MADIWANI WAPONGEZA UONGOZI WA HALMASHAURI YA ARUSHA KWA HATI SAFI YA UKAGUZI
yaani makala yote MADIWANI WAPONGEZA UONGOZI WA HALMASHAURI YA ARUSHA KWA HATI SAFI YA UKAGUZI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MADIWANI WAPONGEZA UONGOZI WA HALMASHAURI YA ARUSHA KWA HATI SAFI YA UKAGUZI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/05/madiwani-wapongeza-uongozi-wa.html
0 Response to "MADIWANI WAPONGEZA UONGOZI WA HALMASHAURI YA ARUSHA KWA HATI SAFI YA UKAGUZI"
Post a Comment