Loading...

MATUMIZI MABAYA YA DAWA ZA UTI HUSABABISHA UZIWI KWA WATOTO

Loading...
MATUMIZI MABAYA YA DAWA ZA UTI HUSABABISHA UZIWI KWA WATOTO - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MATUMIZI MABAYA YA DAWA ZA UTI HUSABABISHA UZIWI KWA WATOTO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MATUMIZI MABAYA YA DAWA ZA UTI HUSABABISHA UZIWI KWA WATOTO
link : MATUMIZI MABAYA YA DAWA ZA UTI HUSABABISHA UZIWI KWA WATOTO

soma pia


MATUMIZI MABAYA YA DAWA ZA UTI HUSABABISHA UZIWI KWA WATOTO

wataalamu wameonya kuwa matumizi yasiyo sahihi ya dawa aina ya Gentamyn inatibu uambukuzi katika njia ya mkojo (UTI), kwa mama wajawazito husababisha tatizo la uziwi kwa watoto wanaozaliwa.

 Takwimu zilizotolewa na Hospitali ya Taifa Muhimbili zinaeleza kuwa zaidi ya 95% ya wagonjwa walioathiriwa na tatizo hilo la uziwi ni watoto wadogo ambao uzaliwa wakiwa hivyo. 


Daktari bingwa wa masikio pua na koo (ENT) kutoka Muhimbili, Edwin Liyombo alisema madhara ya uziwi kwa  watoto hutokana na dawa mbalimbali wanazotumia wajawazito ambazo hugeuka sumu kwa masikio ya watoto. 


Alisema dawa ya Gentamyn iwapo mama anayeumwa UTI ataitumia pasipo kufuata kanuni alizopewa na daktari hugeuka sumu na kuathiri mfumo wamasikio ya mtoto aliye tumboni. "Wanawake wanapokuwa Wajawazito Mara nyingi husumbuliwa na tatizo la maambukizi katika njia ya mkoo na wengine malaria hivyo  mama akitumia Quinnine kutibu malaria hizi Mara nyingi zina sumu , mama akinywa vibaya anaweza kupata tatizo", alisema. 


Dr Liyombo alisema ikiwa mama hatakuwa mwanalifu wakati mtoto anazaliwa na akapata maambukizi katika kitovu, asipotibiwa vizuri pia anaweza kupata tatizo la uziwi. "Ugonjwa wa manjano pia huleta sumu ambayo inaweza kusababisha madhara kwenye  masikio" alisema. 


Kutokana na hatari hiyo mmoja wa wazazi ambao watoto was wamefanyiwa upasuaji,Bupe Mwakalindile  alishauri wazazi kuwa makini na watoto kwani kuna umri ukifika mtoto lazima awe amejua mambo kadhaa ikiwamo kujifunza kuzungumza hivyo wakiona hana dalili wamfikishe kwa wataalam haraka ili afanyiwe vipimo na kuwekewa kifaa cha kumsaidia.


"Nilipopata taarifa za mtoto wangu kuwa na ulemavu wa kusikia nilijisikia vibaya, ukiangalia safari ya mimba miezi 9 mpaka kujifungua halafu unakutana na wataalamu wanakwambia mtoto kiziwi. Ila tunashukuru alipata tiba na yupo vizuri sasa anasoma chekechea ila kuna changamoto nyingi kwa kweli," alisema Bupe. 


Kuhusu tiba ya upasuaji, Dk Liyombo alisema Muhimbili itaanza rasmi kutoa huduma hiyo kwa watoto wasiosikia na kuwawekea vifaa vya usikivu (cochlea implant) mwezi ujao. 


"Gharama imekuwa ni kubwa kwa mzazi kutoka hapa kwenda India tukafikiria nini tunaweza kufanya ili kusaidia. Tulishaanza kufanya Mipango ya kusogeza Huduma kwa kuanza na matengenezo ya vifaa walivyowekewa 'mapping' tunaendelea na sasa tunakuja na upasuaji kufikia juni" alisema.


Dk Liyombo ambaye pia ni Mkuu wa idara ya masikio pua na koo (ENT) alisema gharama za kupandikiza kifaa cha usikivu kwa mtoto mmoja ni kati ya sh80 hadi 100 milion anapopelekwa nje ya nchi.


Source: Mwananchi 13/05/2017


Hivyo makala MATUMIZI MABAYA YA DAWA ZA UTI HUSABABISHA UZIWI KWA WATOTO

yaani makala yote MATUMIZI MABAYA YA DAWA ZA UTI HUSABABISHA UZIWI KWA WATOTO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MATUMIZI MABAYA YA DAWA ZA UTI HUSABABISHA UZIWI KWA WATOTO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/05/matumizi-mabaya-ya-dawa-za-uti.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MATUMIZI MABAYA YA DAWA ZA UTI HUSABABISHA UZIWI KWA WATOTO"

Post a Comment

Loading...