Loading...

KESI YA WEMA SEPETU KUENDELEA KUSIKILIZWA MWAKANI.

Loading...
KESI YA WEMA SEPETU KUENDELEA KUSIKILIZWA MWAKANI. - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa KESI YA WEMA SEPETU KUENDELEA KUSIKILIZWA MWAKANI., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : KESI YA WEMA SEPETU KUENDELEA KUSIKILIZWA MWAKANI.
link : KESI YA WEMA SEPETU KUENDELEA KUSIKILIZWA MWAKANI.

soma pia


KESI YA WEMA SEPETU KUENDELEA KUSIKILIZWA MWAKANI.


Tokeo la picha la picha ya WEMA


Kesi ya matumizi ya dawa za kulevya inayomkabili Mlimbwende wa Tanzania mwaka 2006 na msanii maarufu wa Filamu nchini,  Wema Sepetu  itaendelea kusikilizwa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka Januari mwaka kesho.

Kesi hiyo iliyoko katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo ilipaswa kuendelea kusikilizwa  mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ambapo Wakili wa Serikali, Costantine Kakula alieleza kuwa wapo tayari kwa ajili ya kuendelea na ushahidi na wana mashahidi wawili.

Hata hivyo wakili wa utetezi, Devotha Kianga aliyekuwa akimuwakilisha wakili Peter Kibatala aliomba kesi hiyo iahirishwe hadi tarehe nyingine

kwa kuwa wakili Kibatala  ambaye anamtetea, wema na wenzake wawili, yuko Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi kwenye kesi namba 85 ya mwaka 2016.

Kutokana na maelezo hayo, Hakimu Simba aliiahirisha kesi hiyo hadi Januari 10, 2018.

Washtakiwa wengine wanaoshtakiwa pamoja na Wema, ni Angelina Msigwa  na Matrida Seleman Abbas. Kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa na kiwango kidogo cha dawa za kulevya na kutumia dawa za kulevya.

Inadaiwa  kuwa  Februari 4, 2017 katika Makazi ya Wema huko Kunduchi Ununio  washtakiwa hao walikutwa na msokoto mmoja na vipisi vya bangi vyenye uzito wa gramu 1.08.

Kwa upande wa Wema yeye anadaiwa kuwa Februani Mosi, 2017 katika  eneo lisilojulikana jijini Dar es Salaam,  alitumia dawa za kulevya  aina ya Bangi.


Wema ni miongoni mwa watu waliotajwa na Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Paul Makonda wakituhumiwa kujihusisha na dawa za kulevya.


Inadaiwa kuwa Februari 3, 2017, Wema alijipeleka mwenyewe katika Kituo cha Polisi Kati ambapo alikamatwa.
 Na Karama Kenyunko,


Hivyo makala KESI YA WEMA SEPETU KUENDELEA KUSIKILIZWA MWAKANI.

yaani makala yote KESI YA WEMA SEPETU KUENDELEA KUSIKILIZWA MWAKANI. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala KESI YA WEMA SEPETU KUENDELEA KUSIKILIZWA MWAKANI. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/12/kesi-ya-wema-sepetu-kuendelea_12.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "KESI YA WEMA SEPETU KUENDELEA KUSIKILIZWA MWAKANI."

Post a Comment

Loading...