Loading...

TAAZIA (OBITUARY) BURIANI MZEE KITWANA KONDO

Loading...
TAAZIA (OBITUARY) BURIANI MZEE KITWANA KONDO - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TAAZIA (OBITUARY) BURIANI MZEE KITWANA KONDO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TAAZIA (OBITUARY) BURIANI MZEE KITWANA KONDO
link : TAAZIA (OBITUARY) BURIANI MZEE KITWANA KONDO

soma pia


TAAZIA (OBITUARY) BURIANI MZEE KITWANA KONDO

Na Ramadhan K. Dau
Siku ya Jumatano tarehe 24 Mei 2017 ni siku ambayo itakumbukwa na Watanzania wengi na haswa Waislamu kwa kuondokewa na mzee wetu Alhaj Kitwana Selemani Kondo maarufu “KK” au mzee wa mjini. 

Siku 4 kabla ya kifo chake, mwanawe wa kiume Bwana Adnan Kitwana Kondo maarufu “Saku” alinitumia ujumbe kwenye WhatsApp akiniarifu kuwa mzee KK amelazwa Hindu Mandal na hali ya afya yake inazidi kuzorota. Siku ya pili yake nilimtumia ujumbe “Saku” kutaka kujua hali ya mzee inaendeleaje. Majibu ya “Saku” yaliniashiria kuwa mzee wetu amekaribia kufika mwisho wa safari yake. Aliniambia kuwa kwa sababu ya ukaribu wangu na mzee KK hana budi aniarifu ukweli ulivyo. Aliniarifu kuwa hali ya mzee ni mbaya sana na kwamba kinachosubiriwa na Rehma Zake Mwenyezi Mungu. Kwa kweli ujumbe ule ulihuzunisha sana na sikuweza kuhimili uchungu ule peke yangu. Nikamwarifu Profesa Hamza Mustafa Njozi, Makamu Mkuu wa Chuo cha Waislamu Morogoro na Bwana Faraji Abdallah Tamim, mwalimu wa chuoni hapo.
Ilipofika siku ya Jumatano tarehe 24 Mei nikapata taarifa kupitia moja ya kundi sogozi (chat group) kuwa mzee KK amefariki dunia. Pamoja ya kuwa hali hiyo ilikuwa tayari inatawala fikra zangu lakini kifo hakizoeleki.  

Moja kati ya sifa zake nyingi ni ujasiri. Mzee KK hakuwa mwoga na alikuwa na ujasiri wa kusimamia jambo ambalo anaamini ni sahihi na lina manufaa kwa nchi yetu. Mifano iko mingi. Kwa leo itoshe tu kuwa alisimamia suala la upatikanaji wa Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro kwa kujenga hoja kwa Rais wa wakati huo Mhe Benjamin William Mkapa mpaka Mhe Rais akashawishika kuwa ni jambo jema kuanzishwa kwa chuo hicho kwenye majengo ya kilichokuwa Chuo cha Mafunzo cha TANESCO.
(Pichani ni Mhe Mkapa akiwa na KK kushoto kwake na viongozi wengine waliohudhuria sherehe ya kuzindua uanzishwaji wa Chuo cha Kiislamu Morogoro).  
Kama kuna mtu mmoja ambaye ametoa mchango wa kipekee uliopelekea upatikanaji wa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM) mtu huyo ni mzee Kitwana Kondo. 

Kwa kuenzi jitihada zake hizo, na kwa kuzingatia mzee Kondo ni Mwenyekiti mwanzilishi wa Taasisi ya Maendeleo ya Waislamu (MDF), taasisi ambayo ndiyo Mmiliki wa MUM, nashauri uongozi wa Chuo utafute jengo lenye hadhi pale Chuoni lipewe jina lake. Kwa siku za usoni, Chuo kitakapoanza kutoa shahada za Uzamivu (PhD), nashauri mzee Kitwana Kondo atunukiwe PhD (Honoris Causa) posthumously.


Hivyo makala TAAZIA (OBITUARY) BURIANI MZEE KITWANA KONDO

yaani makala yote TAAZIA (OBITUARY) BURIANI MZEE KITWANA KONDO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TAAZIA (OBITUARY) BURIANI MZEE KITWANA KONDO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/05/taazia-obituary-buriani-mzee-kitwana.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "TAAZIA (OBITUARY) BURIANI MZEE KITWANA KONDO"

Post a Comment

Loading...