Loading...

WAZALISHAJI WATAKIWA KUHAKIKI UBORA WA BIDHAA ZAO KUPITIA MAABARA ZA TBS

Loading...
WAZALISHAJI WATAKIWA KUHAKIKI UBORA WA BIDHAA ZAO KUPITIA MAABARA ZA TBS - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZALISHAJI WATAKIWA KUHAKIKI UBORA WA BIDHAA ZAO KUPITIA MAABARA ZA TBS, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZALISHAJI WATAKIWA KUHAKIKI UBORA WA BIDHAA ZAO KUPITIA MAABARA ZA TBS
link : WAZALISHAJI WATAKIWA KUHAKIKI UBORA WA BIDHAA ZAO KUPITIA MAABARA ZA TBS

soma pia


WAZALISHAJI WATAKIWA KUHAKIKI UBORA WA BIDHAA ZAO KUPITIA MAABARA ZA TBS


Frank Mvungi
Mwambawahabari
SERIKALI  imewataka wazalishaji na wajasiriamali  nchini kuhakikisha kuwa bidhaa wanazozalisha zinakidhi viwango vya ubora vilivyowekwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ili kuchochea ukuaji wa uchumi.
Kauli hiyo imetolewa Leo Jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Kitengo cha Maabara ya Uhandisi wa  Ujenzi ya Shirika la Viwango Nchini,  Mhandisi Stephen Minja wakati wa ziara ya waandishi wa habari kutembelea na kujionea namna maabara za shirika hilo zinavyotekeleza jukumu lake la kuhakiki viwango vya ubora hapa nchini.
Akifafanua zaidi Minja amesema kuwa mabara za shirika hilo zipo kwa ajili ya kuhudumia wazalishaji wa bidhaa mbalimbali na wale wanaoingiza bidhaa kutoka nje ya nchi  lengo ili kuhakiki ubora wa bidhaa zote ili kuepusha athari zinazoweza kujitokeza kwa watumiaji.
“Maabara yetu ina viwango vya kimataifa na gharama zake ni nafuu ambazo kila mwananchi anaweza kumudu lengo likiwa ni kutoa huduma kwa wananchi na kuchangia kuchochea maendeleo  kwa kudhibiti bidhaa hafifu alisema  Minja
Aliongeza kuwa maabara hiyo inapima bidhaa za ujenzi kama  nondo, chokaa, vigae, mbao, mabomba ya maji, simenti, nguzo za umeme,matofali,zege, mchanga na bidhaa zote zinazotumika katika ujenzi wa barabara ikiwemo lami.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa kitengo cha maabara ya umeme,  Mhandisi Anectus Ndunguru amesema kuwa vifaa vyote vya umeme vinavyozalishwa na kuingizwa nchini lazima vipimwe ubora wake kuona kama vinakidhi vigezo ili kuepusha majanga.
Alitaja baadhi ya vifaa ambavyo lazima vihakikiwe ubora wake kuwa ni vifaa vyote vinavyotumika katika kujenga mfumo wa umeme katika majengo, taa za majumbani, pasi, redio, televisheni, waya .
Akizungumzia athari za kutumia vifaa visvyo na ubora Ndunguru amesema kuwa athari za matumizi ya vifaa hivyo ni makubwa ikiwemo kusababisha majanga na kupotea kwa umeme hivyo kuongeza gharama kwa mtumiaji.
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limekuwa likisisitiza matumizi ya bidhaa zenye ubora na zilizohakikiwa na kuepuka bidhaa hafifu ambazo kwa sasa zimedhibitiwa na shirika hilo kwa kiwango kikubwa hali inayochochea ukuaji wa sekta ya Viwanda hapa nchini.


Hivyo makala WAZALISHAJI WATAKIWA KUHAKIKI UBORA WA BIDHAA ZAO KUPITIA MAABARA ZA TBS

yaani makala yote WAZALISHAJI WATAKIWA KUHAKIKI UBORA WA BIDHAA ZAO KUPITIA MAABARA ZA TBS Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZALISHAJI WATAKIWA KUHAKIKI UBORA WA BIDHAA ZAO KUPITIA MAABARA ZA TBS mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/05/wazalishaji-watakiwa-kuhakiki-ubora-wa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WAZALISHAJI WATAKIWA KUHAKIKI UBORA WA BIDHAA ZAO KUPITIA MAABARA ZA TBS"

Post a Comment

Loading...