Loading...
title : Benki Ya KCB Tanzania Yachangia Damu
link : Benki Ya KCB Tanzania Yachangia Damu
Benki Ya KCB Tanzania Yachangia Damu
Wafanyakazi wa Benki ya KCB Bank Tanzania leo wamechangia damu. Hii ni katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya uchangiaji damu (world blood donor day) ambayo itaadhimishwa dunia nzima jumatano wiki hii, tarehe 14 Juni.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo ambalo lilihudhuriwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Ummy Mwalimu, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Cosmas Kimario alisema kuwa mchango huo upo ndani ya vipaumbele vya benki katika uwekezaji jamii kwa ajili ya kusaidia jamii zilizo na uhitaji.
“Benki ya KCB Tanzania inadhamini uwajibikaji kwa jamii ambayo kwa kiwango kikubwa inalenga maeneo ya vipaumbele vya Afya, Elimu Mazingira, Ujasiriamali na malengo yake hasa ni kujikita katika masuala ya ubinadamu” alisema Kimario.
Mkurugenzi huyo alisema kuwa swala la kuchangia damu ni la muhimu sana kwani kuna wagonjywa wengi wenye hitaji la damu hivyo elimu juu ya uchangiaji damu salama ni muhimu kutolewa kwa jamii ili kuifanya jamii kuwa na uelewa mpana juu ya zoezi hilo.
“Tumeamua kuandaa uchangiaji wa damu ili kuisaidia serikali katika sekta ya Afya hususani katika kupunguza vifo vinavyotokana na upungufu wa damu” aliongeza Kimario.
Akizungumza katika zoezi hilo Waziri Ummy Mwalimu aliipongeza Benki ya KCB Tanzania kwa mchango wake huo na kutoa wito kwa wadau wengine kuiga mfano wa ukarimu wa Benki hiyo, akibainisha kwamba serikali inahitaji kubwa la damu hivyo inawahamasisha na kuwakaribisha watanzania wengi zaidi kujitokeza kuchangia damu na kuokoa maisha kwa kuwa serikali haiwezi kufanikisha malengo peke yake.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Mh. Ummy Mwalimu (kulia) akiongea na waandishi wa habari (hawamo pichani) kuhusiana na zoezi la uchangiaji damu salama na kuipongeza Benki ya KCB kwa kushiriki katika zoezi hilo lililofanyika Makao Makuu ya benki hyo jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya KCB Bw. Cosmas Kimario.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Mh. Ummy Mwalimu (kushoto) akimpongeza mmoja wa wafanyakazi wa Benki ya KCB Bi. Francisca Alphonce kwa kuwa mmoja wa watanzania waliojitokeza kuchangia damu salama
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Mh. Ummy Mwalimu (wapili kushoto) kwenye picha ya pamoja na sehemu ya timu ya menejimenti ya Benki ya KCB Tanzania na baadhi ya wakilishi kutoka wizarani. Timu ya menejimenti ya Benki ya KCB, Wapili kulia ni Bw. Cosmass Kimario, wakwanza kulia ni Bw. Masika Mukule, wakwanza kushoto ni Bi. Christine Manyenye, wakwanza kushoto juu ni Bi. Joyce Wiki Mwashigadi na watatu kulia juu ni Bw. Rojas Mdoe.
Hivyo makala Benki Ya KCB Tanzania Yachangia Damu
yaani makala yote Benki Ya KCB Tanzania Yachangia Damu Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Benki Ya KCB Tanzania Yachangia Damu mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/06/benki-ya-kcb-tanzania-yachangia-damu.html
0 Response to "Benki Ya KCB Tanzania Yachangia Damu"
Post a Comment