Loading...
title : MAKAMU WA RAIS AWASILI BUTIAMA,KESHO KUWA MGENI RASMI KILELE CHA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI
link : MAKAMU WA RAIS AWASILI BUTIAMA,KESHO KUWA MGENI RASMI KILELE CHA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI
MAKAMU WA RAIS AWASILI BUTIAMA,KESHO KUWA MGENI RASMI KILELE CHA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewasili mkoani Mara alasiri ya leo 3-June-2017 akitokea mkoani Mwanza ambapo hapo kesho atakuwa ni mgeni rasmi katika kilele cha Siku ya Mazingira Duniani.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka shada la maua juu ya kaburi la Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mara baada ya kuwasili Butiama ambapo atakuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za siku ya mazingira Duniani ambazo Kitaifa zinafanyika Butiama mkoani Mara.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa heshima mbele ya kaburi la Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mara baada kuweka shada la maua,Makamu wa Rais yupo Butiama kuhudhuria sherehe za siku ya mazingira Duniani ambazo Kitaifa zinafanyika Butiama mkoani Mara.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye kikao cha kupokea taarifa ya mkoa wa Mara mara baada ya kuwasili Butiama kwenye makazi ya Hayati Baba wa Taifa.
.............................................................................
Alipowasili kijijini Butiama, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amepokelewa na Viongozi wa vyama vya siasa na watendaji mbalimbali wa Serikali ambao wameongozwa na Mkuu wa mkoa wa Mara Dkt Charles Mlingwa pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira January Makamba.
Makamu wa Rais pia amepokea taarifa ya maendeleo ya mkoa wa Mara na amepata fursa ya kuwasha mshumaa na kuweka shada la maua katika kaburi la baba wa Taifa Hayati Julius Nyerere lililopo Mwitongo kijijini Butiama.
Hapo kesho tarehe 4-June-2017 Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ataongoza mamia ya wananchi wa mkoa wa Mara na mikoa ya Jirani katika Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambapo kitaifa sherehe hizo zitafanyika katika kijiji cha Butiama mkoani Mara.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka shada la maua juu ya kaburi la Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mara baada ya kuwasili Butiama ambapo atakuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za siku ya mazingira Duniani ambazo Kitaifa zinafanyika Butiama mkoani Mara.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa heshima mbele ya kaburi la Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mara baada kuweka shada la maua,Makamu wa Rais yupo Butiama kuhudhuria sherehe za siku ya mazingira Duniani ambazo Kitaifa zinafanyika Butiama mkoani Mara.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye kikao cha kupokea taarifa ya mkoa wa Mara mara baada ya kuwasili Butiama kwenye makazi ya Hayati Baba wa Taifa.
.............................................................................
Hivyo makala MAKAMU WA RAIS AWASILI BUTIAMA,KESHO KUWA MGENI RASMI KILELE CHA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI
yaani makala yote MAKAMU WA RAIS AWASILI BUTIAMA,KESHO KUWA MGENI RASMI KILELE CHA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAKAMU WA RAIS AWASILI BUTIAMA,KESHO KUWA MGENI RASMI KILELE CHA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/06/makamu-wa-rais-awasili-butiamakesho.html
0 Response to "MAKAMU WA RAIS AWASILI BUTIAMA,KESHO KUWA MGENI RASMI KILELE CHA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI"
Post a Comment