Loading...

TADB: “ATAKAYE NA AJE KUKOPA”

Loading...
TADB: “ATAKAYE NA AJE KUKOPA” - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TADB: “ATAKAYE NA AJE KUKOPA”, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TADB: “ATAKAYE NA AJE KUKOPA”
link : TADB: “ATAKAYE NA AJE KUKOPA”

soma pia


TADB: “ATAKAYE NA AJE KUKOPA”


Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB) imewahakikisha kuwapatia mikopo wakulima wa Zao la Karafuu visiwani Zanzibar katika kuhakikisha inachangia kwa kiasi kikubwa katika kuleta Mapinduzi yenye tija katika wakulima hao.

Hayo yalielezwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga wakati akitoa mada juu ya fursa zinazopatikana kwa ajili ya wakulima na wadau wa kilimo cha karafuu visiwani Zanzibar katika Kikao cha Wadau wa Karafuu kilichokuwa kinafanyika mjini Unguja.

Bw. Assenga alisema kuwa Serikali inatambua changamoto wanazokutana nazo wakulima nchini na hivyo uanzishwaji wa TADB unalenga kutekeleza hatua mbalimbali zikilenga kuharakisha mapinduzi na maendeleo katika Sekta ya Kilimo ikiwemo uendelezaji wa zao la karafuu ambalo ni zao kuu la biashara visiwani Zanzibar.

“Tunatambua kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) iliweka Mkakati Maalum wa miaka 10 (2011 -2021) wa kuongeza uzalishaji, usafirishaji, ubora na tija wa zao la karafuu kwa kutambua hilo Benki inakuja kuongeza kasi juhudi hizi za Serikali,” alisema.

Alisema kwa kutambua juhudi za SMZ zao la karafuu lilipewa kipaumbele cha pekee miongoni mwa minyororo ya thamani ya kwanza kuanza kupatiwa mikopo na Benki hiyo kwa ajili ya uongezaji wa thamani mazao mbalimbali nchini.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (kushoto) akimsikiliza Katibu na Mwanasheria wa Shirika la Taifa la Biashara Zanzibar (ZSTC), Bw. Ali Hilali Vuai (kulia) wakati wa Kikao cha Wadau wa Karafuu ambapo TADB ilialikwa kuwasilisha mada. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Taifa la Biashara Zanzibar (ZSTC), Bw. Kassim Maalim Suleiman (kushoto) akizungumza wakati wa Kikao cha Wadau wa Karafuu ambapo TADB ilialikwa kuwasilisha mada juu ya fursa zinazopatikana kwa ajili ya wakulima na wadau wa kilimo cha karafuu. 
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga akiwasilisha mada juu ya fursa zinazopatikana kwa ajili ya wakulima na wadau wa kilimo cha karafuu wakati wa Kikao cha Wadau wa Karafuu visiwani Zanzibar. 
Meneja wa Shirika la Taifa la Biashara Zanzibar (ZSTC), Bw. Ali Usi (kulia) akifafanua jambo kwa Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo wa TADB, Bw. Augustino Chacha (katikati).



Hivyo makala TADB: “ATAKAYE NA AJE KUKOPA”

yaani makala yote TADB: “ATAKAYE NA AJE KUKOPA” Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TADB: “ATAKAYE NA AJE KUKOPA” mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/05/tadb-atakaye-na-aje-kukopa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "TADB: “ATAKAYE NA AJE KUKOPA”"

Post a Comment

Loading...