Loading...

Milioni 20 za Biko zaenda kwa Ramadhan wa Dodoma

Loading...
Milioni 20 za Biko zaenda kwa Ramadhan wa Dodoma - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Milioni 20 za Biko zaenda kwa Ramadhan wa Dodoma, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Milioni 20 za Biko zaenda kwa Ramadhan wa Dodoma
link : Milioni 20 za Biko zaenda kwa Ramadhan wa Dodoma

soma pia


Milioni 20 za Biko zaenda kwa Ramadhan wa Dodoma

DONGE nono la Sh Milioni 20 la bahati nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’, droo ya 16, leo limeenda kwa mshindi wao Ramadhan Juma Hussein, mwenye maskani yake mjini Dodoma, ikiwa ni mara ya kwanza kwa Makao Makuu ya Nchi ya Tanzania kupata mshindi wake katika droo kubwa inayofanyika Jumatano na Jumapili.

Ushindi wa Ramadhan umekuja siku chache baada ya kukabidhiwa fedha zake mshindi wa Handeni, mkoani Tanga, Yahaya Ally Khamis, aliyekabidhiwa pesa mapema wiki hii.

Akizungumza katika droo hiyo leo mchana, Balozi wa Biko, Kajala Masanja alimpongeza Ramadhan kwa kuibuka na ushindi mnono wa Sh Milioni 20, huku akiwataka Watanzania wote kucheza kwa wingi na mara nyingi ili wazoe mamilioni ya Biko.

“Naomba kutangaza kwamba mshindi wetu wa Jumatano hii wa Sh Milioni 20 ni Ramadhan anayetokea mjini Dodoma, ambaye pia amekiri kucheza Biko mara kwa mara pamoja kuwahi kushinda zawadi za papo kwa hapo ambao zinatoka kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja zinatoka kila dakika kwa wale wanaocheza bahati nasibu yetu.

Mchezo huu unachezwa kwa kupitia ujumbe mfupi wa maandishi kwenye mitandao ya simu ya Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel, ambao huingiza namba ya kampuni ambayo ni 505050 na ile ya kumbukumbu 2456, baada ya kufanya muamala kuanzia Sh 1,000 na kuendelea na kupata nafasi ya kuwania zawadi za papo kwa hapo bila kusahau kuingia kwenye droo kubwa ya Sh Milioni 20,” Alisema Kajala.

Naye Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema Biko imezidi kukolea baada ya kumpata mshindi wa Dodoma kwa mara ya kwanza tangu waanze kuchezesha bahati nasibu yao, huku akiwapongeza wote waliowahi kushinda donge nono la Biko kutoka kwenye mikoa mbalimbali ya Tanzania.

“Ni furaha kubwa kuona Dodoma wameibuka na donge nono la Biko, huku nikiamini kuwa kucheza Biko ni rahisi pamoja na kuweza kuibuka na ushindi wa zawadi za papo hapo bila kusahau zawadi kubwa ya Sh Milioni 20 inayotoka mara mbili kwa wiki,” Alisema Heaven.

Balozi wa Biko Kajala Masanja kulia akiwa kwenye tukio la kumtafuta mshindi wa Sh Milioni 20 wa droo ya 16 ya Biko, ambapo bwana Ramadhan Hussein wa Dodoma aliibuka kidedea na kuzoa kiasi hicho cha pesa kutoka Biko. Kushoto ni mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Emmanuel Ndaki.


Hivyo makala Milioni 20 za Biko zaenda kwa Ramadhan wa Dodoma

yaani makala yote Milioni 20 za Biko zaenda kwa Ramadhan wa Dodoma Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Milioni 20 za Biko zaenda kwa Ramadhan wa Dodoma mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/06/milioni-20-za-biko-zaenda-kwa-ramadhan.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Milioni 20 za Biko zaenda kwa Ramadhan wa Dodoma"

Post a Comment

Loading...