Loading...
title : Mkutano wa Sita wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar waahirishwa
link : Mkutano wa Sita wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar waahirishwa
Mkutano wa Sita wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar waahirishwa
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameonya kwamba kuanzia sasa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haitowavumilia Madaktari wanaofanya uzembe wakati wa kutoa huduma za Afya kwa Wananchi wanafika Hospitalini kupata huduma za matibabu.
Alisema Serikali haitosita kumfukuza kazi mara moja Daktari ye yote atakayebainika kufanya uzembe wa makusudi bila ya kujali jina au sifa alizonazo Daktari husika.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa onyo hilo wakati akitoa hoja ya kuahirisha Mkutano wa Sita wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar lililojadili Bajeti ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Mwaka 2017/2018 kwenye ukumbi wa Baraza hilo Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Alisema dhamira ya Serikali kupitiA Wizara husika ya Afya ni kutoa huduma bora yaliyobainishwa na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakati wakichangia Hotuba ya Wizara ya Afya.
Balozi alisema yapo malalamikombali mbali ya kiutendaji hasa katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja yaliyojitokeza ambayo huleta kero na maudhi kwa Wananchi wanaofika kupata huduma za matibabu.
Alitanabahisha wazi kwamba baadhi ya Madaktari wamekuwa na tabia sugu ya kutotekeleza wajibu na majukumu yao wakati wengine wakipenda kutumia lugha chafu zinazowavunja moyo wagonjwa.
Alisema hatua hiyo inakera na kuchukiza Wananchi kutokana na kufikia huduma zinazotolewa kamwe hazilingani na fedha nyingi zinazotolewa na kugharamiwa na Serikali kwa kila Mwezi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alitahadharisha kwamba vipo vifaa kufanyia uchunguzi kwa wagonjwa ambavyo kufanyiwa hujuma kwa makusudi ili wahusika wawaelekeze wagonjwa kwenda kwenye Hospitali zao au zile wanazopewa baghshishi.
Alisema kitendo hicho kisichokubalika si cha haki kufanyiwa wagonjwa ambao wengi wao ni maskini na baadhi yao hutoka masafa ya mbali kama Vijijini kufuata huduma za matibabu Hospitali za rufaa.
Akizungumzia migogoro ya ardhi Zanzibar licha ya Serikali kuanzisha Kamisheni ya ardhi kwa lengo la kuodnosha migogoro hiyo kupitia Mamlaka ya Ardhi Balozi Seif alisema bado tatizo hilo halijapatiwa ufumbuzi kutokana na baadhi ya Watu hawajali kufuata sheria.
Alisema hivi sasa Kamisheni ya Ardhi ipo katika hatua za kutayarisha Sera mpya ya Ardhi, kuweka usimamizi imara wa Ardhi pamoja na upangaji wa matumizi bora ya Ardhi.
Balozi Seif alieleza kwamba Serikali kufuta maeneo yote ya Ardhi ili yarudi Serikalini na kupangwa upya.
Alifahamisha kwamba kuanzia sasa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haitomvumilia mtu ye yote ambae atasababisha migogoro ya Ardhi hata kama ni Kiongozi au Mwananchi wa kawaida.
Baraza la Wawakilishi limeahirishwa hadi asubuhi ya Jumatano ya Tarehe 27 Septemba Mwaka huu wa 2017.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiufunga Mkutano wa Sitai wa Baraza la Tisa laWawakilishi Zanzibar uliokuwa ukijadili Bajeti ya Serikali ya mwaka 2017/2018 katika Ukumbi wa Baraza hilo uliopo Chukwani nje kidogo ya Kusini mwa Mji wa Zanzibar.
Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Baadhi ya Waheshimiwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakifuatilia Hotuaba ya Balozi Seif katika Baraza la Wawakilishi Chukwani.
Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakichukuwa dondoo kwenye Hotuba ya kufungwa kwa Mkutano wa Sita wa Baraza la Tisa la Wawakilishi iliyotolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hayupo pichani.
Wa kwanza kulia ni Mh. Simai Mohammed Said Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu. Mh.Suleiman Sarahan Said Mwakilishi wa Jimbo la Chake chake na Mwakilishi wa Kuteuliwa Ikulu Mheshimiwa Ahmeda Abdulwakil.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe.Zuberi Ali Maulid akitoka barazani baada ya kuahirishwa Mkutano wa Sita wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar lililojadili Bajeti ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Mwaka 2017/2018 kwenye ukumbi wa Baraza hilo Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Hivyo makala Mkutano wa Sita wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar waahirishwa
yaani makala yote Mkutano wa Sita wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar waahirishwa Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Mkutano wa Sita wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar waahirishwa mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/06/mkutano-wa-sita-wa-baraza-la-tisa-la.html
0 Response to "Mkutano wa Sita wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar waahirishwa"
Post a Comment