Loading...
title : Mradi wa HIPZ Waandaa Resi za Baskeli Kukusanya Fedha Kwa Ajili ya Kuimarisha Huduma za Afya Hospitali ya Makunduchi na Kivunge Zanzibar.
link : Mradi wa HIPZ Waandaa Resi za Baskeli Kukusanya Fedha Kwa Ajili ya Kuimarisha Huduma za Afya Hospitali ya Makunduchi na Kivunge Zanzibar.
Mradi wa HIPZ Waandaa Resi za Baskeli Kukusanya Fedha Kwa Ajili ya Kuimarisha Huduma za Afya Hospitali ya Makunduchi na Kivunge Zanzibar.
Na Ramadhani Ali – Maelezo Zanzibar.
Mradi wa Kuimarisha huduma za Afya Zanzibar (HIPZ) unatarajia kukusanya zaidi ya dola za Marekani 25,000 kwa ajili ya kusaidia huduma za afya katika Hospitali ya Makunduchi na Kivunge ambazo wanazisaidia.
Fedha hizo zitapatikana kufuatia kuandaa resi za baiskeli za kilomita 300 (Bike Ride 2017) katika mikoa mitatu ya Unguja yatakayo dumu kwa muda wa siku sita kuanzia leo.
Akizungumza na waandishi wa habari Hoteli ya Tembo, Mratibu wa resi hizo Dkt. Jon Rees kutoka Uingereza amesema jumla ya wapanda baiskeli 25 kutoka Ulaya na Zanzibar wanashiriki.
Amesema fedha hizo zitachangwa na makampuni ya ndani na nje ya nchi na zitatumika kuimarisha huduma za afya hasa afya ya mama na mtoto katika Hospitali za Kivunge na Makunduchi.
Amesema Resi hizo ambazo ni mara ya tatu kufanya Zanzibar zilianzia Mji Mkongwe kuzunguka maeneo mbali mbali ya Mkoa Mjini Magharibi zitapitia Nungwi, Makunduchi, Kizimkazi na zitrejea Mji Mkongwe.
Dkt. Ress amewataka wananchi wa Zanzibar kuwaunga mkono na kuwatia hamasa wapanda baiskeli hao hasa katika sehemu watakazopita.
Akizindua resi hizo, Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Dkt. Fadhil Abdalla Mohd amesema Mradi wa HIPZ umeleta mafanikio makubwa katika ubunifu wake wa kutafuta fedha kwa ajili ya huduma za afya kwa kuanzisha mbio hizo.
Amesema pamoja na kukusanya fedha kwa ajili ya huduma za afya pia mbio hizo ni sehemu ya kuwashawishi vijana kufanya mazoezi ambayo ni moja ya njia ya kujikinga na maradhi yasiyoambukiza.
Dkt. Fadhil amesema wakati serikali ipo katika mpango wa kuzipandisha daraja Hospitali ya Makunduchi na Kivunge kuwa za Mkoa, fedha hizo zitatumika kuanzisha majengo mapya na kuimarisha huduma za afya.
Hivyo makala Mradi wa HIPZ Waandaa Resi za Baskeli Kukusanya Fedha Kwa Ajili ya Kuimarisha Huduma za Afya Hospitali ya Makunduchi na Kivunge Zanzibar.
yaani makala yote Mradi wa HIPZ Waandaa Resi za Baskeli Kukusanya Fedha Kwa Ajili ya Kuimarisha Huduma za Afya Hospitali ya Makunduchi na Kivunge Zanzibar. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Mradi wa HIPZ Waandaa Resi za Baskeli Kukusanya Fedha Kwa Ajili ya Kuimarisha Huduma za Afya Hospitali ya Makunduchi na Kivunge Zanzibar. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/06/mradi-wa-hipz-waandaa-resi-za-baskeli.html
0 Response to "Mradi wa HIPZ Waandaa Resi za Baskeli Kukusanya Fedha Kwa Ajili ya Kuimarisha Huduma za Afya Hospitali ya Makunduchi na Kivunge Zanzibar."
Post a Comment