Loading...
title : SHINDANO LA SPRITE BBALL KINGS LAINGIA HATUA YA 16 BORA
link : SHINDANO LA SPRITE BBALL KINGS LAINGIA HATUA YA 16 BORA
SHINDANO LA SPRITE BBALL KINGS LAINGIA HATUA YA 16 BORA
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Shindano la Sprite Bball Kings 2017 limeingia katika hatua ya 16 baada ya timu 52 kukipiga wikiendi hii ikiwa ni ufunguzi wa michuano hiyo.
Michezo hiyo 26 iliyochezwa katika viunga vya viwanja vya Jakaya M Kikwete Park (JKM Park) na kuzikutanisha timu hizo 52 katika mechi 26 za mtoano na 16 kufanikiwa kuingia hatua inayofuata.
Akitoa tathmini ya michuano hiyo Mratibu wa Sprite Bball Kings Basilisa Biseko amesema kuwa hatua ya mtoano imefanyika wikiendi hii na timu 16 kufanikiwa kuingua hatua inayofuata ila katika mechi hizo kuna baadhi walipewa ushindi wa mezani.
Basilisa amesema kuwa kuna baadhi ya timu hazikufanikiwa kufika siku hiyo na ratiba ilikuwa tayari imeshapangwa katika droo iliyokuwa imepangwa na kupelekea timu iliyokuwa imefika uwanjani kupatiwa ushindi wa mezani.
"Katika michezo 26 iliyochezwa siku ya Jumamosi katika viwanja vya JMK Park timu 16 zimefanikiwa kuingia hatua ya 16 bora, ila kuna timu zingine zimeingia kwenye hatua hiyo bila kucheza na timu pinzani kutokana na mpinzani wake kutokufika na kupelekea kupewa alama zitakazomruhusu kuingia hatua inayofuata,"amesema Basilisa.
Amesema kuwa, kwa timu zilizopata alama nyingi ndizo zilizofanikiwa kuingia katika hatua ya 16 bora na mashindano hayo yataendelea tena ili kumpata mshindi wa Sprite Bball Kitaa kwa mwaka 2017.
Timu zilizofuzu kuingia hatua ya 16 bora katika shindano la Sprite Baball Kings 2017 ni DMI, Dream Chaser, UDSM, Oysterbay, Ukonga Warriors, The Fighter, Ardhi na Bongo Hits.
Timu zingine ni Chanika Legends, Montfort, Heroes S/B, Kigamboni Heroes, TMT, Mchenga, Kurasini na Landforce.
Mashindano ya Bball Kings mwaka huu yanadhaminiwa na Sprite wakishirikiana na kituo cha East Africa Redio na TV na yalizinduliwa mapema mwezi wa tano na kuanza usaili kwa wilaya za Teemek, Kindondoni na Ilala na kupata timu 4.52 zilizojitokeza kushiriki shindano hilo.
Timu ya mpira wa kikapu ya UDSM wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mtanange wao.
Timu ya mpira wa kikapu ya UDSM (jezi ya njano) wakipambana katika hatua ya mtoano ya shindano la Sprite Bball Kings iliyofanyika mwishoni mwa wiki hii katika viwanja vya Jakaya M Kikwete Park (JKM Park).
Mashabiki na timu zingine zilizoshiriki katika hatua ya mtoano ya shindano la Sprite Bball Kings iliyofanyika mwishoni mwa wiki hii katika viwanja vya Jakaya M Kikwete Park (JKM Park) wakiwa jukwaani wakifuatilia baadhi ya michezo mingine.
Timu za mpira wa kikapu wakiwa wanachuana katika shindano la Sprite Bball Kings iliyofanyika mwishoni mwa wiki hii katika viwanja vya Jakaya M Kikwete Park (JKM Park).
Kamishna wa Ufundi na Uendeshaji Mashindano wa chama Shirikisho la Mpira wa Kikapu (TBF) na Mratibu wa Sprite BBall Kings Manase Zablon (kushoto) akiwa pamoja na mtangazaji wa East African Drive David Rweganyira wakichambua baadhi mechi zilizokuwa zikiendelea.
Hivyo makala SHINDANO LA SPRITE BBALL KINGS LAINGIA HATUA YA 16 BORA
yaani makala yote SHINDANO LA SPRITE BBALL KINGS LAINGIA HATUA YA 16 BORA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SHINDANO LA SPRITE BBALL KINGS LAINGIA HATUA YA 16 BORA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/06/shindano-la-sprite-bball-kings-laingia.html
0 Response to "SHINDANO LA SPRITE BBALL KINGS LAINGIA HATUA YA 16 BORA"
Post a Comment