Loading...
title : ASKOFU GAVILLE ASEMA, KATIBA MPYA NDIYO MUAROBAINI WA UFISADI
link : ASKOFU GAVILLE ASEMA, KATIBA MPYA NDIYO MUAROBAINI WA UFISADI
ASKOFU GAVILLE ASEMA, KATIBA MPYA NDIYO MUAROBAINI WA UFISADI
KUKAMILIKA kwa mchakato wa uaandaaji wa Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutasaidia kuweka misingi imara na kuondoa changamoto zilizopo katika Katiba ya sasa, hivyo kukomesha ufisadi na kuinua uchumi wa Tanzania.
Aidha, kukamilika huko kwa Katiba Mpya kutaakisi jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli.
Hayo yalisemwa hivi karibuni na Askofu Mteule wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Iringa, Blaston Gaville, ambaye alimtaka Rais Magufuli kuumalizia mchakato wa kuandikwa kwa Katiba Mpya, kwani alisema mbali ya kuakisi kasi yake anayoifanya ya kukuza uchumi pia kutasaidia kuhimiza uwajibikaji.
“Wakristo na Watanzania kwa ujumla tuna imani kubwa na Serikali ya Awamu ya Tano na ni matarajio yetu kwamba mchakato wa kuandika Katiba utamalizwa kama lengo lilivyokuwa,” alisema.
Askofu Gaville amesimikwa ili kuchukua nafasi ya Askofu Dkt. Owdenburg Mdegella ambaye amestaafu.Alisema wanatiwa moyo na jitihada zinazoendelea kufanywa na Dkt. Magufuli katika kufufua uchumi na kuhakikisha rasilimali za nchi zinatumika kwa manufaa ya Watanzania wote.
Askofu Mteule wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Iringa, Blaston Gaville (kushoto).
Askofu Blaston Gaville wakati akiwekwa wakfu kuongoza Dayosisi ya Iringa ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT).
Hivyo makala ASKOFU GAVILLE ASEMA, KATIBA MPYA NDIYO MUAROBAINI WA UFISADI
yaani makala yote ASKOFU GAVILLE ASEMA, KATIBA MPYA NDIYO MUAROBAINI WA UFISADI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala ASKOFU GAVILLE ASEMA, KATIBA MPYA NDIYO MUAROBAINI WA UFISADI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/07/askofu-gaville-asema-katiba-mpya-ndiyo.html
0 Response to "ASKOFU GAVILLE ASEMA, KATIBA MPYA NDIYO MUAROBAINI WA UFISADI"
Post a Comment