Loading...

HOTUBA YA WAMJW KATIKA UFUNGUZI WA MKUTANO WA KWANZA NA KUPITIA UTEKELEZAJI WA MKAKATI WA UBORESHAI WA KAZI YA UIBUAJI WA WAGONJWA WA KIFUA KIKUU NCHINI TAREHE 4 JULAI, 2017

Loading...
HOTUBA YA WAMJW KATIKA UFUNGUZI WA MKUTANO WA KWANZA NA KUPITIA UTEKELEZAJI WA MKAKATI WA UBORESHAI WA KAZI YA UIBUAJI WA WAGONJWA WA KIFUA KIKUU NCHINI TAREHE 4 JULAI, 2017 - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa HOTUBA YA WAMJW KATIKA UFUNGUZI WA MKUTANO WA KWANZA NA KUPITIA UTEKELEZAJI WA MKAKATI WA UBORESHAI WA KAZI YA UIBUAJI WA WAGONJWA WA KIFUA KIKUU NCHINI TAREHE 4 JULAI, 2017, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : HOTUBA YA WAMJW KATIKA UFUNGUZI WA MKUTANO WA KWANZA NA KUPITIA UTEKELEZAJI WA MKAKATI WA UBORESHAI WA KAZI YA UIBUAJI WA WAGONJWA WA KIFUA KIKUU NCHINI TAREHE 4 JULAI, 2017
link : HOTUBA YA WAMJW KATIKA UFUNGUZI WA MKUTANO WA KWANZA NA KUPITIA UTEKELEZAJI WA MKAKATI WA UBORESHAI WA KAZI YA UIBUAJI WA WAGONJWA WA KIFUA KIKUU NCHINI TAREHE 4 JULAI, 2017

soma pia


HOTUBA YA WAMJW KATIKA UFUNGUZI WA MKUTANO WA KWANZA NA KUPITIA UTEKELEZAJI WA MKAKATI WA UBORESHAI WA KAZI YA UIBUAJI WA WAGONJWA WA KIFUA KIKUU NCHINI TAREHE 4 JULAI, 2017


Image result for picha za ummy mwalimu



HOTUBA YA MHESHIMIWA UMMY MWALIMU (MB), WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO KATIKA UFUNGUZI WA MKUTANO WA KWANZA WA KUPITIA UTEKELEZAJI WA MKAKATI WA UBORESHAJI WA KASI YA UIBUAJI WA WAGONJWA WA KIFUA KIKUU NCHINI, KATIKA UKUMBI WA KILIMANI LANDMARK, DODOMA, JULAI 4, 2017


  • Katibu Mkuu wamjw,
  • Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI ,
  • Mganga Mkuu Kiongozi,
  • Wajumbe kutoka Global Fund,
  • Wakurugenzi na Wawakilishi wa USAID, CDC, EGPAF, AGPAHI, Save the Children, FHI, MDH, AMREF, KNCV, Delloite, Baylor, Water Reeds na wengine,
  • Wakurugenzi kutoka TAMISEMI na WAMJW,
  • Mameneja Mipango ya NTLP, RCH na NACP,
  • Waganga Wakuu wa Mikoa na Waganga Wakuu wa Wilaya,
  • Waratibu wa Mikoa na Wilaya wa TB na Ukoma na TBHIV,
  • Watoa huduma kutoka Vituo vya Afya katika Halmashauri,
  • Waandishi wa Habari,
  • Waalikwa wote,
  • Mabibi na Mabwana.
Awali ya yote nitumie fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kutujalia afya njema na kutuwezesha kukutana hapa. Pili, niwashukuru waandaaji kwa kunialika katika mkutano huu muhimu; mkutano wa kwanza wa kitaifa wa kufanya mapitio ya utekelezaji wa mkakati wa uboreshaji wa kasi ya uibuaji wa wagonjwa wa kifua kikuu. Hii ni hatua muhimu kujiangalia na kuona njia tunayopitia katika juhudi za kuhakikisha tunawafikia kila mwenye uhitaji wa huduma za matibabu ya kifua kikuu. Vile vile, nitumie fursa hii kuwakaribisha wajumbe wote na nawapongeza kwa kuchukua muda wenu kuja kuhudhuria kikao kazi hiki muhimu. Natambua pia ya kuwa kuna wajumbe wengine wamesafiri umbali mkubwa na wengine wametoka nje ya nchi; “napenda kusema wote karibuni sana hapa Dodoma, makao makuu ya nchi yetu”.
Wageni Waalikwa, Mabibi na Mabwana,
Utoaji wa huduma za afya usiozingatia ubora huathiri kila mtu, si tu wateja na wagonjwa wetu, hata sisi watoa huduma. Huduma zikiwa mbovu zinawafanya hata wanaozihitaji kukata tamaa na kutojitokeza vituoni. Malengo Endelevu ya Maendeleo na mkakati wa Dunia wa kutokomeza kifua kikuu (End TB Strategy)  yametilia mkazo utoaji wa huduma za afya zenye ubora wa hali ya juu na kwamba si budi juhudi za makusudi kufanyika ili kila mhitaji kufikiwa. Masuala ya ubora wa huduma za afya yamepewa kipaumbele katika mkakati mpya uliotolewa na Shirika la Afya Duniani wa kutokomeza kifua kikuu ifikapo mwaka 2035. Wakati huo huo, kikao cha Baraza la Shirika la Afya Duniani kilochoketi mwezi uliopita kimeziagiza nchi wanachama na Shirika la Afya Duniani (WHO) kutilia mkazo wa kipekee mipango yakinifu ya ubora katika utoaji huduma zote za afya. Kikao hicho, kimewataka wahisani na mashirika yenye uwezo kuzisaidia nchi zenye uhitaji ili kuzijengea ujuzi wa kuboresha misingi ya huduma bora za afya.
Wageni Waalikwa, Mabibi na Mabwana,
Changamoto kubwa tuliyonayo hapa kwetu Tanzania, ni kutoweza kuifikia sehemu kubwa ya wagonjwa wa kifua kikuu. Kiasi cha wagonjwa zaidi ya 100,000 wa kifua kikuu hatuwafikii kila mwaka. Licha ya kuwa na mazingira yaliyosawa na maeneo mengine mfano katika Mikoa ya Rukwa, Katavi, Simiyu, Shinyanga, Kigoma, Kagera, Dodoma, Iringa, Mara na Singida inagundua wagonjwa wachache sana ikilinganishwa na Mikoa ya Mbeya, Lindi, Mtwara na Tanga.  Tafiti nyingi zimeonyesha kwamba, tunahitaji mbinu mpya za kuboresha huduma tunazozitoa ili kuhakikisha kila mgonjwa na mteja anayekuja katika vituo vyetu vya huduma anapata fursa ya kuchunguzwa kikamilifu ili kubaini kama anaugua kifua kikuu au la.
Wageni Waalikwa, Mabibi na Mabwana,
Mkakati wa uboreshaji kasi ya uibuaji wagonjwa wa kifua kikuu ni mkakati uliojaa mbinu za kiuendeshaji ili kuvipa uwezo vituo vyetu vya huduma kufanya uchunguzi wa kina kwa kila mteja anayepata huduma vituoni na kuwapata wote wenye kuugua kifua kikuu na kuwaanzishia matibabu. Mathalan, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma katika miezi sita baada ya kuanza kutekeleza mkakati huu wameongeza wastani wa kuibua wagonjwa wa kifua kikuu kutoka 28 hadi 54 kwa mwezi. Tunahitaji kubadili mtazamo wetu na utendaji kazi wetu hasa suala zima la  kuhakikisha tunafanya upekuzi na uchunguzi wa wagonjwa vituoni, tusingoje mgonjwa atufuate na kutueleza dalili za kifua kikuu akiwa kituoni, hivyo ni vyema juhudi zetu zianzie kuwatambua wagonjwa hawa katika jamii.

Wageni Waalikwa, Mabibi na Mabwana,
Ili kuhakikisha tunaweka misingi mizuri ya utekelezaji wa mkakati huu, Wizara ikishirikiana na Global Fund, imetengeneza kitita kiongozi ili kutoa mwongozo kwa watoa huduma katika kila kitengo na kliniki ndani ya vituo vya huduma jinsi ya kufanya hatua kwa hatua kubaini kifua kikuu kwa kila mwenye kugua bila kukosa. Mkakati huu muhimu unatoa fursa kwa kila kitengo kujitathmini ili kuweka misingi timilifu ya uchunguzi wa kifua kikuu kwa wateja wote wanaohudhuria matibabu katika eneo lao. Kitita hiki kinaviwezesha vituo vyetu vya huduma kumfikia kila mmoja mwenye uhitaji wa uchunguzi wa kifua kikuu, kutoa huduma zinazozingatia usawa, usalama wa mgonjwa au mteja na huduma zinazokidhi viwango vya Kimataifa.
Wageni Waalikwa, Mabibi na Mabwana,
Tunao wajibu wa kuhakikisha mkakati huu unatekelezwa kwa ufanisi uliokusudiwa, ili tufikie lengo hilo, Wizara kwa mara ya kwanza imeanzisha rejesta mpya ya wanaohisiwa kuwa na kifua kikuu itakayowekwa katika kila ngazi ya utoaji wa huduma za Afya hapa nchini. Tayari rejesta hizi zimesambazwa na kuanza kutumika katika mikoa 16 iliyoanza kutekeleza zoezi hili. Kesho kutwa, wote hapa tutashuhudia kuzinduliwa kwa mkakati huu maalumu wa uboreshaji huduma za uibuaji wagonjwa wa kifua kikuu katika Halmashauri.  Zana hizi zitatoa mwanga na kuangaza njia bora za kuchunguza kifua kikuu na kubaini wote wenye kuugua katika jamii yetu mijini na vijijini. Mafanikio endelevu ya mkakati huu, yanategemea jinsi tutakavyojipanga kuanzia ngazi ya zahanati hadi wasimamizi ngazi ya kitaifa katika Wizara ya Afya na TAMISEMI. Mbinu zinazoelekezwa ni za kawaida, nyepesi na zinaeleweka vizuri na utekelezaji wake utaleta matokeo chanya na unaweza kufikiwa na kila mtoa huduma. Kazi zilizoainishwa katika kutekeleza mkakati huu zinatoa chagizo kwa watoa huduma vituoni na wasimamizi kuwajibika kikamilifu, kila mmoja katika nafasi yake na kujenga timu imara katika kila eneo la kazi.
Wageni Waalikwa, Mabibi na Mabwana,
Nimetaarifiwa kuwa, utekelezaji wa mkakati huu ulianza mnamo Julai, 2016, ambapo ni mwaka mmoja sasa tokea vituo vya mwanzo katika Mikoa ya Mbeya na Dodoma ianze kuweka msukumo mpya. Kuanzia hapo, Mikoa 16, wilaya 48 na vituo 187 nchini kote vimeweza kuanza utekelezaji. Katika mkutano huu wa kwanza wa kufanya mapitio na tathmini ya utekelezaji wa mkakati huu, ninafarijika kuwa umehudhuriwa na wajumbe wa RHMT na CHMT na watumishi kutoka vituo vya huduma katika Mikoa hiyo yote 16 ambao wote ni walengwa wakuu katika kufanikisha jukumu hili.
Wageni Waalikwa, Mabibi na Mabwana,
Napenda kubainisha changamoto mbili kuu tunazo hitaji kukabiliana nazo, Moja, kuanzisha mfumo imara wa ufuatiliaji na usimamizi elekezi, Pili, ni kuhakikisha tunatoa usimamizi imara na wenye tija katika kuimarisha ufanyaji kazi kama timu ya ushindi na kuvifanya vituo vyetu kutoa huduma kwa wagonjwa wa kifua kikuu zilizo za bora na endelevu. Kufikia hatua hizi yatubidi kuimarisha timu za uboreshaji huduma vituoni (Quality Improvement teams – QIT) na kuzipa uwezo zaidi wa kusimamia viwango vya ubora wa huduma za afya katika maeneo yao ya kazi vituoni, hospitali na vituo vya ngazi za chini pia.


Wageni Waalikwa, Mabibi na Mabwana,
Napenda kuwaaminisha ya kuwa, tukiweza kuwabaini wale wanaofanya vizuri zaidi katika vituo vilivyo katika Halmashauri zetu na tukawatumia kueneza utendaji wao mzuri katika maeneo mengine inaweza kuleta matokeo chanya kwa haraka na kupata mafanikio endelevu. Watendaji bingwa hawa, watatusaidia kurahisisha hatua za ugatuzi na kupanua huduma hizi katika nchi nzima. Ili mpango huu ulete mafanikio tunayoyatarajia, inabidi timu za uendeshaji za Mikoa na Halmashauri kuwapa kila msaada ili wafanye vizuri zaidi na kuimarisha ubora wa mfumo mzima wa afya katika maeneo yetu.

Wageni Waalikwa, Mabibi na Mabwana,
Mkakati huu na utekelezaji wa kazi nyingine za kuimarisha mfumo wetu wa huduma bora za afya hatuwezi kuvifanya peke yetu; yatubidi kuzitelekeleza katika ushirika wa pamoja kati ya Serikali na wadau wetu. Ni napenda kutumia fursa hii, kuwashukuru wadu wetu wa maendeleo kwa ushirikiano na misaada mnayoendelea kutupatia. Wote kwa pamoja tunawashukuru sana.
Hitimisho:
Kwa mara nyingine tena nitumie fursa hii kuwashukuru wadau wa maendeleo kwa kutusaidia kuimarisha miundo mbinu ya Afya, mifumo ya uendeshaji huduma za afya na udhibiti wa magonjwa mbali mbali yakiwemo UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria. Ni imani yangu pia ya kuwa ushikaino huu utazidi kuimarika na kusonga mbele ili tuweze kuboresha utoaji wa huduma za Afya. Ni imani yangu vile vile kwamba kongamano hili ni fursa ya kipekee kubadilishana uzoefu wa namna ya kutenda kazi kwa ufanisi wa hali ya juu katika kuibua mbinu bunifu mbali mbali ili kuboresha huduma katika mikoa na Halmashauri zetu.
Baada ya kusema haya machache, sasa napenda kutamka rasmi kuwa, mkutano huu umefunguliwa.
Asanteni kwa kunisikiliza.


Hivyo makala HOTUBA YA WAMJW KATIKA UFUNGUZI WA MKUTANO WA KWANZA NA KUPITIA UTEKELEZAJI WA MKAKATI WA UBORESHAI WA KAZI YA UIBUAJI WA WAGONJWA WA KIFUA KIKUU NCHINI TAREHE 4 JULAI, 2017

yaani makala yote HOTUBA YA WAMJW KATIKA UFUNGUZI WA MKUTANO WA KWANZA NA KUPITIA UTEKELEZAJI WA MKAKATI WA UBORESHAI WA KAZI YA UIBUAJI WA WAGONJWA WA KIFUA KIKUU NCHINI TAREHE 4 JULAI, 2017 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala HOTUBA YA WAMJW KATIKA UFUNGUZI WA MKUTANO WA KWANZA NA KUPITIA UTEKELEZAJI WA MKAKATI WA UBORESHAI WA KAZI YA UIBUAJI WA WAGONJWA WA KIFUA KIKUU NCHINI TAREHE 4 JULAI, 2017 mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/07/hotuba-ya-wamjw-katika-ufunguzi-wa.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "HOTUBA YA WAMJW KATIKA UFUNGUZI WA MKUTANO WA KWANZA NA KUPITIA UTEKELEZAJI WA MKAKATI WA UBORESHAI WA KAZI YA UIBUAJI WA WAGONJWA WA KIFUA KIKUU NCHINI TAREHE 4 JULAI, 2017"

Post a Comment

Loading...