Loading...
title : MAGEREZA KUPANUA KIWANDA CHAKE CHA VIATU CHA KARANGA MJINI MOSHI
link : MAGEREZA KUPANUA KIWANDA CHAKE CHA VIATU CHA KARANGA MJINI MOSHI
MAGEREZA KUPANUA KIWANDA CHAKE CHA VIATU CHA KARANGA MJINI MOSHI
Jeshi la Magereza nchini limeanza kutekeleza mpango wake wa kupanua shughuli za uzalishaji wa kiwanda cha Viatu cha Karanga kilichopo mjini Moshi mkoani Kilimanjaro sambamba na kujenga Kiwanda Kipya cha Viatu katika eneo hilo hilo ili kupanua huduma zake kwa wananchi na hivyo kukidhi mahitaji ya soko la sasa.
Hatua hii ni moja ya kati ya Mikakati ya Jeshi la Magereza nchini Tanzania linaloongozwa na Kamishna Jenerali Dk. Juma Malewa (Pichani juu), kuhakikisha fursa zilizopo na wataalamu waliopo ndani ya Jeshi la Magereza nchini zinatumika na wanatumika vizuri kwa manufaa ya watanzania wote sambamba na Jeshi hilo kushiriki kikamilifu katika kuhakikisha Tanzania inafikia uchumi wa viwanda.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, Dr. Juma Malewa anasema baada ya upanuzi huo ambao umeanza kufanyika mapema mwezi Juni mwaka huu kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha jozi 400 kwa siku na hivyo kuongeza kasi ya upatikanaji wa viatu vinavyotengenezwa na Jeshi la Magereza kwa ubora kwa hali ya juu na kwa kutumia mitambo ama mashine za kisasa.
Dk. Malewa anasema awali kiwanda hicho kilichopo Gereza la Karanga mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro kutokana na kutumia teknolojia ya zamani kilikuwa na uwezo wa kuzalisha jozi 150 kwa siku kiwango ambacho ni kidogo ukilinganisha na soko la sasa.
Anasema tayari Jeshi la Magereza limeingia Ubia na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa PPF kwa lengo la kupanua shughuli za uzalishaji wa Kiwanda cha Viatu cha Karanga kilichopo mjini Moshi mkoani Kilimanjaro sambamba na kujenga kiwanda kipya cha viatu katika eneo hilo hilo.
Dk. Malewa anasema katika kutekeleza azma yake ya ujenzi wa Kiwanda kipya cha Viatu tayari zimetengwa ekari 20 kwa ajili ya kiwanda hicho katika eneo hilo la Karanga mjini Moshi na kwamba eneo hilo hilo litakalotumika kujenga Kiwanda cha Viatu pia litatumika kujenga Kiwanda cha Soli na Kiwanda cha kuchakata Ngozi na kwamba Kiwanda hicho kinategemewa kukamilika mapema Julai mwaka 2018.
Hivyo makala MAGEREZA KUPANUA KIWANDA CHAKE CHA VIATU CHA KARANGA MJINI MOSHI
yaani makala yote MAGEREZA KUPANUA KIWANDA CHAKE CHA VIATU CHA KARANGA MJINI MOSHI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAGEREZA KUPANUA KIWANDA CHAKE CHA VIATU CHA KARANGA MJINI MOSHI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/07/magereza-kupanua-kiwanda-chake-cha.html
0 Response to "MAGEREZA KUPANUA KIWANDA CHAKE CHA VIATU CHA KARANGA MJINI MOSHI"
Post a Comment