Loading...
title : MBUNGE GULAMALI AFANYA ZIARA YA JIMBONI KWAKE
link : MBUNGE GULAMALI AFANYA ZIARA YA JIMBONI KWAKE
MBUNGE GULAMALI AFANYA ZIARA YA JIMBONI KWAKE
Mbunge wa Jimbo la Manonga, Seif Khamis Gulamali akizungumza na wananchi wa kata ya Ntobo kaskazini iliyoko katika Wilaya ya Igunga Mkoa wa Tabora katika moja ya ziara yake leo. wa pili kulia ni Diwani wa kata hiyo, Emmanuel Samson. (Picha zote na Raymond Urio)
Caps 3
Mbunge wa Jimbo la Manonga, Seif Khamis Gulamali akisikiliza maoni ya wananchi wa kata ya Ntobo kaskazini iliyoko katika Wilaya ya Igunga Mkoa wa Tabora katika moja ya ziara yake leo. kulia kwake ni Diwani wa kata hiyo, Emmanuel Samson.
Caps 4
Mbunge wa Jimbo la Manonga, Seif Khamis Gulamali akizungumza na wananchi wa kata ya Mwashiku iliyoko katika Wilaya ya Igunga Mkoa wa Tabora katika moja ya ziara yake leo.
Mbunge wa Jimbo la Manonga, Seif Khamis Gulamali akizungumza na wananchi wa kata ya Choma iliyoko katika Wilaya ya Igunga Mkoa wa Tabora katika moja ya ziara yake leo.
mwambawahabariblog
Mbunge wa Jimbo la Manonga kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Seif Khamis Gulamali leo amefanya ziara katika kata ya Ntobo Kaskazini, Ngulu, Mwashiku na Choma kwenye Wilaya ya Manonga jana ikiwa ni sehemu ya kutekeleza ilani ya Chama hicho.
Awali Mbunge Gulamali aliwasili katika kata ya Ntobo Kaskazini na kujionea maendeleo yanayoendelea kwenye kata hiyo na kuhaidi kuendelea kutoa huduma kadiri inavyowezekana. Hata hivyo Mbunge Gulumali alitoa shukrani kwa wanachi wote walio weza kumchagua ili kuwa mbunge wao na kuweza kuwatumikia.
'Na washukuru wananchi wote wa Kata ya Ntobo kwa kuweza kunichagua na kuwa kiongozi wenu hivyo wajibu wangu ni kuendelea kuwahudumia kama niliweza kuhaidi. alisema Gulumali.
Hata hivyo Gulumali amechangia mabati 20 pamoja na mbao 50 za ujenzi wa ofisi za Chama hicho katika Kata hiyo. Lakini pia Diwani wa kata hiyo Emmanuel Samson alitoa shukrani kama sehemu ya kuwawakilisha waanachi wa kata hiyo kwa msaada huo pamoja na kuhaidi kumuunga mkono Mbunge huyo.
Hata hivyo Mbunge Gulamali aliweza pia kuwatembelea wanachi wa kata ya Ngulu, kwa kuangalia maendeeo yanayoendelea baada ya awali kuchangia fedha kwaajili ya ukarabati wa barabara ya barabara kwenye kata hiyo.
Lakini pia Gulamali amehaidi kuchangia mifuko ya seruji kwa ajili ya kutengeneza choo cha Hospitali na nyumba ya Mganga Mkuu katika Hosptali ya kata.
Hata hivyo Gulamali aliweza pia kutembelea wananchi wa kata ya Choma pamoja na Mwashiku na kuwaeleza juu ya ufufuaji wa kiwanda cha Manonga kilichokuwa kimetelekezwa na Mmiliki Rajaan wa kiwanda hicho kwamuda mrefu bila hata kufanya kazi.
Lakini pia aliwahaidi pindi kiwanda hicho kitakapo fufuliwa itakuwa ni nafasi nzuri kwa wananchi wa Choma pamoja na wengine walio katika Wilaya ya Igunga ili waweze kupata kazi katika kiwanda hicho na kuweza kuendesha maisha yao na familia zao.
Hivyo makala MBUNGE GULAMALI AFANYA ZIARA YA JIMBONI KWAKE
yaani makala yote MBUNGE GULAMALI AFANYA ZIARA YA JIMBONI KWAKE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MBUNGE GULAMALI AFANYA ZIARA YA JIMBONI KWAKE mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/07/mbunge-gulamali-afanya-ziara-ya-jimboni.html
0 Response to "MBUNGE GULAMALI AFANYA ZIARA YA JIMBONI KWAKE"
Post a Comment