Loading...
title : Mchezaji yoso wa kikapu kupata mafunzo ya NBA Afrika Kusini
link : Mchezaji yoso wa kikapu kupata mafunzo ya NBA Afrika Kusini
Mchezaji yoso wa kikapu kupata mafunzo ya NBA Afrika Kusini
Balozi wa mchezo wa mpira wa kikapu nchini, Jokate Mwegelo ametoa rai kwa wasichana na wazazi kuwaruhusu watoto wa kike kushiriki katika michezo mbalimbali ili kukuza vipaji na kujiingizia kipato.
Jokate alitoa rai hiyo wakati wa kukabidhi bendera kwa mchezaji chipukizi wa mpira wa kikapu nchini, Jesca Julius Ngaise ambaye anaondoka leo kwenda nchini Afrika Kusini kushiriki katika mafunzo ya juu mchezo huo yatakayoendeshwa na makocha wa kimataifa wa ligi ya NBA ya Marekani.
Amesema kuwa Jesca ambaye ni mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Juhudi ya Ukonga, amepata nafasi hiyo baada ya kuchaguliwa na jopo la makocha na kuweka historia ya kuwa msichana wa kwanza wa Tanzania kuhudhuria mafunzo hayo.
“Hii ni faraja kwa Tanzania, makocha wa kimataifa wameona kipaji cha Jesca ambaye ni nahodha wa timu ya Taifa ya wasichana ya wachezaji wa chini ya miaka 16, ameiwezesha Tanzania kushika nafasi ya tatu katika mashindano ya Afrika Mashariki nchini Kenya, sasa tunampa bendera na kuiwakilisha nchi katika kozi hiyo, ni sifa kubwa kwake na kwa Taifa,”
Balozi wa mchezo wa mpira wa kikapu nchini, Jokate Mwegelo akikabidhi bendera ya Taifa kwa mchezaji Chipukizi, Jesca Ngaise (katikati) wakati wa hafla fupi iliyofanyika kwenye kituo cha michezo za Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park. Anayeshuhudia zoezi hilo ni Kocha maarufu wa mpira wa kikapu Tanzania, Bahati Mgunda.
Balozi wa mchezo wa mpira wa kikapu, Jokate katika picha ya pamoja na baadhi ya wachezaji chipukizi wa mpira wa kikapu kwenye viwanja vya JMK Park.
Baba Mzazji wa Jesca, Julius Ngaise akizungumza
Hivyo makala Mchezaji yoso wa kikapu kupata mafunzo ya NBA Afrika Kusini
yaani makala yote Mchezaji yoso wa kikapu kupata mafunzo ya NBA Afrika Kusini Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Mchezaji yoso wa kikapu kupata mafunzo ya NBA Afrika Kusini mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/07/mchezaji-yoso-wa-kikapu-kupata-mafunzo_29.html
0 Response to "Mchezaji yoso wa kikapu kupata mafunzo ya NBA Afrika Kusini"
Post a Comment