Loading...
title : RC MAKONDA AMEKABIDHIWA GARI AINA YA WINGLE 5 NA KAMPUNI YA GREAT WALL MOTORS
link : RC MAKONDA AMEKABIDHIWA GARI AINA YA WINGLE 5 NA KAMPUNI YA GREAT WALL MOTORS
RC MAKONDA AMEKABIDHIWA GARI AINA YA WINGLE 5 NA KAMPUNI YA GREAT WALL MOTORS
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amekabidhiwa gari aina ya Wingle 5 na Kampuni ya Great Wall Motors ya nchini China kwa kushirikiana na kampuni ya wazawa ya Kifaru Motors (T).
Akielezea sababu ya kukabidhi gari hiyo kwa serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam Meneja Mwandamizi wa Kampuni hiyo nchini Afrika Kusini Jianguo Liu ameeleza kuwa ni kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli.
Meneja Liu ameeleza kuwa gari hiyo inathamani ya shilingi milioni 55, hivyo itumike kutatua changamoto mbalimbali.
Kwa upande wake RC Makonda amewashukuru wahisani hao kwa msaada huo na kuahidi kuutumia msaada huo kama ilivyokusudiwa, huku akieleza kuwa utaratibu wa kulitumia gari hilo utatokana na maoni ya wananchi ambapo watapiga kura kupitia namba maalumu na kueleza gari hilo liende kwenye idara ipi, kwa mfano idara ya elimu, afya, polisi nakadhalika, zoezi hilo litachukua siku kumi.
RC Makonda ameongeza kuwa serikali yake itaendelea na utaratibu huo wa kupigia kura magari yaende kwenye idara ipi ili kuchochea ufanisi wa kazi na wanachi ndiyo watakao kuwa waamuzi wa hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akikabidhiwa gari na Meneja Mwandamizi wa Kampuni hiyo GWM ya nchi ya Afrika Kusini Jianguo Liu leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akilikagua gari hilo.
Muonekano wa gari hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari juu ya kuwashukuru wahisani Kampuni ya Great Wall Motors ya nchini China kwa kushirikiana na kampuni ya wazawa ya Kifaru Motors (T).kwa kukabidhi gari leo jijini Dar es Salaam.
Meneja Mwandamizi wa Kampuni hiyo GWM ya nchi ya Afrika Kusini Jianguo Liu kakizungumza machache kabla ya kukabidhi gali hilo leo jijini Dar es Salaam. Picha na Emmauel Massaka,Globu ya Jamii.
Hivyo makala RC MAKONDA AMEKABIDHIWA GARI AINA YA WINGLE 5 NA KAMPUNI YA GREAT WALL MOTORS
yaani makala yote RC MAKONDA AMEKABIDHIWA GARI AINA YA WINGLE 5 NA KAMPUNI YA GREAT WALL MOTORS Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RC MAKONDA AMEKABIDHIWA GARI AINA YA WINGLE 5 NA KAMPUNI YA GREAT WALL MOTORS mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/07/rc-makonda-amekabidhiwa-gari-aina-ya.html
0 Response to "RC MAKONDA AMEKABIDHIWA GARI AINA YA WINGLE 5 NA KAMPUNI YA GREAT WALL MOTORS"
Post a Comment