Loading...
title : Wafanyakazi Benki ya NMB Kilosa wamnunulia mguu wa bandia mtoto mlemavu
link : Wafanyakazi Benki ya NMB Kilosa wamnunulia mguu wa bandia mtoto mlemavu
Wafanyakazi Benki ya NMB Kilosa wamnunulia mguu wa bandia mtoto mlemavu
WAFANYAKAZI wa Benki ya NMB wilayani Kilosa, Morogoro kwa kushirikiana na Kitengo cha Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) cha benki hiyo wametoa msaada kwa mtoto Sheila Bushiri (7) ambaye alizaliwa akiwa mlemavu wa mguu mmoja kufanyiwa upasuaji na kumnunulia mguu wa bandia ili aweze kutembea kama watu wengine.
Akizungumza kuhusu msaada huo, Meneja wa tawi la benki ya NMB KIlosa, Dismas Prosper alisema walimjua mtoto huyo kupitia Bi. Shalphina Lipinga ambaye alikwenda ofisini kwao kuomba msaada wa kusaidia watoto wenye uhitaji na baada ya kuwaonyesha mtoto huyo waliona kuna haja ya kumsaidia.
Alisema baada ya kumwona wao kama wafanyakazi walichangishana pesa na kutokana na utaratibu wa benki hiyo kuwa iwapo wafanyakazi wakichangishana pesa kitengo cha CSR kuwaongezea pesa sawa na kiwango walichotoa walifanikisha mtoto huyo kufikishwa kwenye hospitali ya CCBRT iliyopo Dar es Salaam ambapo alipatiwa matibabu.
“Alikuja ofisini Shalphina kusema kuwa anasaidia watoto ambao hawajiwezi na katika maongezi alisema kuna mtoto alizaliwa na ulemavu wa mguu mmoja na anaishi na bibi yake na anampeleka shule kila siku akimbeba mgongoni hivyo kama kuna mvua hawezi kwenda shule, mimi nikaona hapo kuna shida kubwa, “Nilipoona picha hana mguu mmoja kama mzazi iliniuma sana, niliweza kuwasilisha kwa wafanyakazi wenzangu na nilipowauliza nini tumfanyie wengi walipendekeza baiskeli na tukakubaliana kuchanga, alipopelekwa CCBRT walishauri apate mguu wa bandia na wafanyakazi wengi wakalikubali,” alisema Prosper.
Prosper alisema lengo la wafanyakazi hao kutoa msaada ni kumwona mtoto huyo akiwa na furaha na kuendelea na masomo yake vizuri na kwasasa wana mpango wa kuendelea kutoa msaada kwa watu wengine ambao wanahitaji kupata msaada ili kuendesha shushuli zao za kila siku kama watu wengine ambao hawana ulemavu.
Mwonekano wa mguu wa mtoto Sheila Bushiri kabla ya kusaidiwa na wafanyakazi wa Benki ya NMB Kilosa kufanyiwa upasuaji na kupewa mguu wa bandia.
“Mwisho wa siku tulifanikiwa kuweka tabasamu kwenye uso wa yule mtoto kwa kutumia kile kidogo ambacho Mungu ametusajilia tumsaidie na sio kwa yule mtoto tu tuna malengo ya kuendelea kusaidia wengine ili na wao wapate tabasamu,” alisema Prosper. Kwa upande wa bibi yake Sheila, Habiba Said ambaye ndiyo anaishi na mtoto huyo alisema mtoto huyo alizaliwa na ulemavu huo na akiwa na miezi tisa mama yake alimwacha nyumbani na kuondoka huku baba wa mtoto akiwa hajulikani.
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Hivyo makala Wafanyakazi Benki ya NMB Kilosa wamnunulia mguu wa bandia mtoto mlemavu
yaani makala yote Wafanyakazi Benki ya NMB Kilosa wamnunulia mguu wa bandia mtoto mlemavu Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Wafanyakazi Benki ya NMB Kilosa wamnunulia mguu wa bandia mtoto mlemavu mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/07/wafanyakazi-benki-ya-nmb-kilosa.html
0 Response to "Wafanyakazi Benki ya NMB Kilosa wamnunulia mguu wa bandia mtoto mlemavu"
Post a Comment