Loading...
title : Waharibifu wa Vyanzo vya Maji Kibakwe Kukiona – Waziri Simbachawene
link : Waharibifu wa Vyanzo vya Maji Kibakwe Kukiona – Waziri Simbachawene
Waharibifu wa Vyanzo vya Maji Kibakwe Kukiona – Waziri Simbachawene
Waziri wa Nchi - Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene (kulia) akizungumza na wananchi baada ya kupokea malalamiko yao katika Kijiji cha Lukole kuhusu shida ya maji wanayoipata, wakati alipokwenda kwenye bomba la Kijiji kuzungumza na wakinamama ambao ndio waathirika wakubwa wa tatizo hilo na kuwataarifu namna ambavyo amekwishaanza kushughulikia kero hiyo.
Na Nteghenjwa Hosseah - Kibakwe.
Uharibifu wa vyanzo vya maji ni tatizo lililokithiri katika maeneo mengi Nchini Tanzania huku wananchi wa maeneo hayo wakiendelea kushuhudia na kuvumilia uharibifu huo eti kwa sababu tu wahusika ni ndugu, jamaa ama marafiki wa jamii husika.
Pasipo kujali athari zinazoweza kutokea kutokana na uharibifu wa mazingira hususan vyanzo vya maji wananchi wameendelea kulima, kufuga, kuchunga pamoja na kuishi katika maeneo hayo pasipo kuwa na shaka yoyote na kusababisha ukosefu wa maji kwa jamii inayotegemea vyanzo hivyo.
Athari zaidi zimethibitija katika Kijiji cha Chinyika na Lukole vilovyopo kata ya Chinyika kwa kukosa maji kutokana na Uharibifu uliofanywa na baadhi wa wananchi katika chanzo cha maji kwenye milima ya wota ambacho ndio chanzo kikuu cha maji ya mtiririko kwa wananchi zaidi ya elfu saba.
Waziri wa Nchi - Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene (katikati aliyekaa) akisimikwa kuwa Chifu wa Kigogo katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Kingiti.
Hali hii imepelekea wananchi wa vijiji hivyo vyenye vitongoji zaidi ya kumi na tano kuwekeana zamu ya kuchota maji ambapo kwa wiki kila Kijiji hupata maji kwa siku tatu na kila kaya huchota Ndoo nne kwa siku ya zamu yao ambapo kiasi hicho hakiwajawahi kuwatosha mahitaji ya Kaya.
Wananchi wa Kijiji cha Chinyika wamepaza sauti zao kwa Waziri wa Nchi - Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene wakati wa ziara yake katika vijiji hivyo na kulalamikia tatizo la upungufu wa maji na adha wanayopata kutokana na hali hiyo.
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Hivyo makala Waharibifu wa Vyanzo vya Maji Kibakwe Kukiona – Waziri Simbachawene
yaani makala yote Waharibifu wa Vyanzo vya Maji Kibakwe Kukiona – Waziri Simbachawene Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Waharibifu wa Vyanzo vya Maji Kibakwe Kukiona – Waziri Simbachawene mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/07/waharibifu-wa-vyanzo-vya-maji-kibakwe.html
0 Response to "Waharibifu wa Vyanzo vya Maji Kibakwe Kukiona – Waziri Simbachawene"
Post a Comment