Loading...
title : HAKUNA AJIRA ZILIZOTANGAZWA NA JESHI LA POLISI.
link : HAKUNA AJIRA ZILIZOTANGAZWA NA JESHI LA POLISI.
HAKUNA AJIRA ZILIZOTANGAZWA NA JESHI LA POLISI.
Watu hao wamesambaza taarifa kupitia mitandao ya kijamii inayosomeka ‘Vigezo sifa za kujiunga na Jeshi la Polisi’, huku ndani yake ikitaja sifa ambazo kwa mujibu wa kikundi hicho ndizo anazopaswa kuwa nazo mtu anayeomba nafasi ya kujiunga na Jeshi la Polisi.
Jeshi la polisi linapenda kuwafahamisha wananchi kuwa taarifa hizo ni za uongo na zenye lengo la kupotosha Umma kwa madhumuni wanayoyajua wao wenyewe. Pia zipo taarifa ambazo hazijathibitishwa kuwa wapo watu wanaoombwa kutoa fedha na matapeli hao ili waweze kuwapatia nafasi ya ajira hizo.
Wananchi watambue kuwa Jeshi la Polisi lina utaratibu wake mzuri na wa wazi wa kuajiri. Pale Serikali itakapotoa idhini ya kuajiri watumishi wapya utaratibu huo utatangazwa kwa wananchi ili waweze kuufuata kuomba nafasi hizo.
Jeshi la Polisi linawataka wananchi kutoa taarifa juu ya kikundi hicho kupitia kituo chochote cha Polisi kilicho karibu nawe au ofisi za Serikali ili watu hao waweze kukamatwa na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.
Wananchi mnashauriwa kupata taarifa sahihi za Jeshi la Polisi kupitia website yake ambayo ni http://ift.tt/1EowbAK au akaunti ya twitter http://www.twitter.com/tanpol pamoja na Facebook http://ift.tt/2vnGrJW
Imetolewa na:
Barnabas David Mwakalukwa - ACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi,
Makao Makuu ya Polisi,
S.L.P. 9141,
Dar es Salaam.
Hivyo makala HAKUNA AJIRA ZILIZOTANGAZWA NA JESHI LA POLISI.
yaani makala yote HAKUNA AJIRA ZILIZOTANGAZWA NA JESHI LA POLISI. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala HAKUNA AJIRA ZILIZOTANGAZWA NA JESHI LA POLISI. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/08/hakuna-ajira-zilizotangazwa-na-jeshi-la.html
0 Response to "HAKUNA AJIRA ZILIZOTANGAZWA NA JESHI LA POLISI."
Post a Comment