Loading...
title : MANISPAA YA DODOMA YATENGA ENEO MAALUM KWA AJILI YA MACHINGA
link : MANISPAA YA DODOMA YATENGA ENEO MAALUM KWA AJILI YA MACHINGA
MANISPAA YA DODOMA YATENGA ENEO MAALUM KWA AJILI YA MACHINGA
NA RAMADHANI JUMA.
HALMASHAURI ya Manispaa ya Dodoma imetenga eneo la Makole D-Center lililoko katikati ya Mji wa Dodoma kuwa eneo rasmi kwa ajili ya wafanyabiashara ndogo maarufu kama Machinga kufanya biashara zao badala ya kupaga bidhaa ovyo mitaani hali inayopelekea kuharibu taswira ya mji.
Hatua hiyo pia itasaidia kuendana na kasi kubwa ya ongezeko la wafanyabiashara hao kuingia Mjini humo kutoka mikoa mbalimbali nchini tangu Serikali ilipohamia rasmi Dodoma ambako ni Makao Makuu ya Nchi.
Akizugumza katika mkutano wa Baraza la Madiwani la kufunga wa fedha uliopita lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika ukumbi wa Manispaa hiyo, Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Godwin aliyewajulisha wajumbe na wananchi kuwa, sasa Manispaa iko katika hatua za mwisho kukamilisha ujenzi wa miundombinu muhimu katika eneo hilo ikiwemo vyoo ili shughuli za biashara zifanyike katika mazingira salama na rafiki.
“Tunatarajia eneo hilo litakuwa tayari kufikia mwisho wa mwezi Agosti au mwanzo wa mwezi Septemba mwaka huu mara moja tutaanza zoezi la kuwahamishia wafanyabiashara hao pale” alifafanua.
Alisema Manispaa inashirikiana kwa karibu na viongozi wa wafanyabiashara hao katika zoezi hilo, na kwamba endapo eneo hilo halitatosha, wafanyabiashara wengine watahamishiwa katika eneo la Chaduru .
Tayari Manispaa ya Dodoma ilishaanza zoezi la kuwaondoa wafanyabiashara wa Matunda na chakula katika maeneo yasiyo rasmi na kuwahamishia katika maeneo rasmi ya masoko ikiwemo soko la Sabasaba, Bonanza, na Tambukareli.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma, Godwin Kunambi akizugumza na wakati wa mkutano wa Baraza la Madiwani la kufunga mwaka wa fedha 2016/2017 uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika ukumbi wa Manispaa ya Dodoma. PICHA NA RAMADHANI JUMA.
Hivyo makala MANISPAA YA DODOMA YATENGA ENEO MAALUM KWA AJILI YA MACHINGA
yaani makala yote MANISPAA YA DODOMA YATENGA ENEO MAALUM KWA AJILI YA MACHINGA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MANISPAA YA DODOMA YATENGA ENEO MAALUM KWA AJILI YA MACHINGA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/08/manispaa-ya-dodoma-yatenga-eneo-maalum.html
0 Response to "MANISPAA YA DODOMA YATENGA ENEO MAALUM KWA AJILI YA MACHINGA"
Post a Comment