Loading...
title : PROF. JANABI AIELEZA MAHAKAMA KUWA MANJI ANA VYUMA KWENYE MOYO
link : PROF. JANABI AIELEZA MAHAKAMA KUWA MANJI ANA VYUMA KWENYE MOYO
PROF. JANABI AIELEZA MAHAKAMA KUWA MANJI ANA VYUMA KWENYE MOYO
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imeelezwa kuwa, mfanyabiashara Yusuf Manji amewekewa vyuma kwenye moyo wake na pia anasumbuliwa na maumivu makali na tatizo la kukosa usingizi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi amesema hayo leo mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa mshitakiwa Yusuf Manji amewekewa vyuma kwenye moyo wake na kwamba anasumbuliwa maumivu makali na kukosa usingizi.
Profesa Janabi amesema hayo wakati akitoa ushahidi wake kama shahidi wa kwanza wa upande wa utetezi kwenye kesi matumizi ya dawa za kulevya inayomkabikli Manji.
Akiongozwa na Wakili wa utetezi, Hajra Mungula, Profesa Janabi amdai, Februari na Julai mwaka huu, mshitakiwa Manji alifikishwa katika taasisi hiyo kati kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya moyo, ambapo kwa mara ya kwanza kulazwa ilikuwa Februari.
Amedai kuwa, mara ya kwanza Manji kupelekwa JKCI alipelekwa kama mgonjwa wa nje, ambapo alitoa historia ya matatizo yake na kupatiwa matibabu, lakini baadae alienda tena kuchunguzwa ndipo ikagundulika kuwa moyo wake ulikuwa na tundu hivyo aliwekewa vyuma kwa ajili ya kusaidia msukumo wa damu lakini baadae Julai mwaka huu alifika tena hospitalini hapo akilalamikia maumivu ya moyo upande wa kushoto ambapo walipochunguza waligundua kuwa vyuma vilivyowekwa kwenye moyo wake vinafanya kazi vizuri na kumpatia dawa za maumivu.
Shahidi huyo alidai kuwa, Manji aliwaeleza kuwa kabla ya kwenda JKCI alikuwa anapatiwa matibabu nchini Marekani , lakini pamoja na tiba mbalimbali walimpatia tena dawa kutoka makundi matatu ambazo hazikumbuki na pia kwa tatizo la kutolala vizuri hatukumtibu sisi bali wakati anachukuliwa historia yake alieleza kuwa alipatiwa dawa za kupunguza maumivu na sindano.
Aidha shahidi huyo amedai, mtu yoyote anayewekewa vyuma akitumia vitu vyovyote kama vile sigara, vyakula vya mafuta au dawa kama Heroine anaweza kuathiri utendaji kazi wa vyuma hivyo na kwamba kabla ya kuwekewa mgonjwa hupewa maelekezo nini atumie na vitu gani asitumie lakini maamuzi ya kutumia dawa za kulevya si ya daktari.
Alipoulizwa juu ya madhara anayoweza kupata mgonjwa wa moyo akitumia dawa za kulevya alisema, Vyuma vinavyowekwa kwenye moyo husaidia kuzibua mishipa ili damu izunguke mwili mzima na kuna masharti kwa mtu anayewekewa vyuma. Athari moja wapo ni kujirudia kwa tatizo na kuziba kwa mishipa.
Kesi hiyo itaendelea kesho.
Hivyo makala PROF. JANABI AIELEZA MAHAKAMA KUWA MANJI ANA VYUMA KWENYE MOYO
yaani makala yote PROF. JANABI AIELEZA MAHAKAMA KUWA MANJI ANA VYUMA KWENYE MOYO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala PROF. JANABI AIELEZA MAHAKAMA KUWA MANJI ANA VYUMA KWENYE MOYO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/08/prof-janabi-aieleza-mahakama-kuwa-manji.html
0 Response to "PROF. JANABI AIELEZA MAHAKAMA KUWA MANJI ANA VYUMA KWENYE MOYO"
Post a Comment