Loading...
title : SERIKALI YARIDHIA WAATHIRIWA WA JANGA LA MOTO SOKO LA SIDO KUENDELEA KUBAKI KATIKA ENEO LAO,NAIBU SPIKA ACHANGIA MILIONI KUMI
link : SERIKALI YARIDHIA WAATHIRIWA WA JANGA LA MOTO SOKO LA SIDO KUENDELEA KUBAKI KATIKA ENEO LAO,NAIBU SPIKA ACHANGIA MILIONI KUMI
SERIKALI YARIDHIA WAATHIRIWA WA JANGA LA MOTO SOKO LA SIDO KUENDELEA KUBAKI KATIKA ENEO LAO,NAIBU SPIKA ACHANGIA MILIONI KUMI
Baada ya Soko la Sido kuteketea kwa moto,hatimaye Serikali Mkoani Mbeya imeridhia Waathirika wa janga la Moto katika soko hilo kuendelea kubaki katika maeneo yao ya awali na kuagizwa kujenga vyumba vya kudumu ili kukabilina na majanga ya moto yanapojitokeza.
Akitoa maelekezo ya serikali,Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla amewaagiza watendaji wa halmashauri kupiga kambi katika eneo la soko la Sido haraka kuanzia siku ya kesho, kwa ajili ya kubuni michoro na mpangilio wa soko hilo ili wafanyabiashara waanze ujenzi na hatimae kuendelea na biashara zaoa kama kawaida.
Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa wilaya ya Mbeya Mjini,Mkoa ikiwa ni pamoja na mbunge wa Jimbo Mbeya Mjini Mh.Joseph Mbilinyi pamoja na Naibu Spika Mhe.Dkt Tulia Ackson ambaye ametoa msaada wa shilingi milioni 10 kwa wathirika hao.Aidha baada ya kutolewa kwa kiasi hicho cha fedha ,Mkutano huo ukaridhiwa kuwa fedha hiyo ibaki kwa Mkuu wa Mkoa huku uongozi wa soko ukipanga matumizi ya fedha hiyo.
Hata hivyo mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh.Makala ameliagiza Jeshi la Zimamoto kuendelea kutoa elimu ya zimamoto,kusambaza vifaa vya kuzuia moto na kuchimba visima vya maji vya ziada katika masoko huku akiwataka viongozi wa ngazi zote za mkoa kuchukua tahadhari za moto kwenye masoko kutokana na ripoti kuonesha chanzo cha janga hilo ni mabaki ya moto uliotokea kwenye moja ya vibanda vya mamalishe waliokuwa ndani ya soko hilo.
Baadhi ya Wananchi wakiwa sambamba na Wafanyabiashara wa soko la Sido-Mwanjelwa,wakifurahia uamuzi uliotoewa na Serikali ya Mkoa wa Mbeya,kuwa Wafanyabiasha hao wabaki katika soko hilo badala ya kuhamishwa katika soko lingine.
Baadhi ya Wananchi wakiwa sambamba na Wafanyabiashara wa soko la Sido,wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh Amos Makalla alipokuwa akizungumza nao kwenye mkutano wa pamoja katika kutoa maamuzi ya kuwa Wafanyabiasha hao wabaki katika soko hilo badala ya kuhamishwa katika soko lingine huku utaratibu wa ujenzi ukiendelea kuwekwa sawa.
Hivyo makala SERIKALI YARIDHIA WAATHIRIWA WA JANGA LA MOTO SOKO LA SIDO KUENDELEA KUBAKI KATIKA ENEO LAO,NAIBU SPIKA ACHANGIA MILIONI KUMI
yaani makala yote SERIKALI YARIDHIA WAATHIRIWA WA JANGA LA MOTO SOKO LA SIDO KUENDELEA KUBAKI KATIKA ENEO LAO,NAIBU SPIKA ACHANGIA MILIONI KUMI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI YARIDHIA WAATHIRIWA WA JANGA LA MOTO SOKO LA SIDO KUENDELEA KUBAKI KATIKA ENEO LAO,NAIBU SPIKA ACHANGIA MILIONI KUMI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/08/serikali-yaridhia-waathiriwa-wa-janga.html
0 Response to "SERIKALI YARIDHIA WAATHIRIWA WA JANGA LA MOTO SOKO LA SIDO KUENDELEA KUBAKI KATIKA ENEO LAO,NAIBU SPIKA ACHANGIA MILIONI KUMI"
Post a Comment