Loading...

SHULE YA GENIUS KINGS YAFANYA MAHAFALI YAKE YA 6 JIJINI DAR

Loading...
SHULE YA GENIUS KINGS YAFANYA MAHAFALI YAKE YA 6 JIJINI DAR - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SHULE YA GENIUS KINGS YAFANYA MAHAFALI YAKE YA 6 JIJINI DAR, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SHULE YA GENIUS KINGS YAFANYA MAHAFALI YAKE YA 6 JIJINI DAR
link : SHULE YA GENIUS KINGS YAFANYA MAHAFALI YAKE YA 6 JIJINI DAR

soma pia


SHULE YA GENIUS KINGS YAFANYA MAHAFALI YAKE YA 6 JIJINI DAR

Mkurugenzi Mkuu wa Shule ya Genius Kings Nusery& Primary School, Machage Kisyeri, (Kulia) akisoma hotuba.

Wakati serikali ya Tanzania inao mkakati wa kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda,wanafunzi wanaohitimu masomo wametakiwa kujiona sehemu ya mkakati huo na kusoma kwa bidii kupata ujuzi wa taaluma mbalimbali ikiwemo kutoogopa kusoma masomo ya hesabu na sayansi.

Ushauri huo umetolewa na daktari bingwa nchini wa magonjwa ya nevu (Neurosurgery) kutoka Chuo Kikuu cha Muhimbili,Profesa Joseph Kahamba, wakati wa mahafali ya darasa la saba ya msingi ya Genius Kings yaliyofanyika Segerea jijini Dar es Salaam .

Profesa Kahamba alisema kuwa nchi yetu bado inakabiliwa na changamoto ya kuwa na wataalamu waliobobea katika nyanja mbalimbali ambapo aliwataka wanafunzi wanaohitimu masomo na waliopo mashuleni na vyuoni kujipanga kuhakikisha wanapata utaalamu wa fani mbalimbali tayari kwa kutumikia taifa la Tanzania.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Aloyce Siame (kulia) akikabidhiwa zawadi ya kikombe na Profesa Joseph Kahamba.

“Wanafunzi waliopo mashuleni na vyuoni mnapaswa kujipanga kwa kuhakikisha mnasoma kwa bidii na kupata ujuzi wa fani mbalimbali kwa kuwa mapinduzi ya kuendeleza taifa letu yanayoendelea yanahitaji wataalamu wa fani mbalimbali na wanaotegemewa kuchukua majukumu hayo hawatoki nje ya nchi bali ni nyinyi vijana wa kitanzania”Alisema Profesa Kahamba.

Aliongeza kusema kuwa kinachotakiwa kwa wanafunzi waliopo mashuleni na vyuoni kujibidisha kusoma kwa bidii na kupata taaluma za fani mbalimbali na wahakikishe wanajiamini na kuhakikisha ndoto zao walizojiwekea zinatimia na wanakuwa na uzalendo wa kuitumikia nchi na kuleta maendeleo chanya katika jamii kupitia elimu waliyoipata.

Profesa Kahamba aliupongeza uongozi wa shule ya Genius Kings kwa kufanya uwekezaji katika sekta ya elimu kwa kuwa umelenga kuunga mkono jitihada za serikali za kuboresha elimu nchini na kuleta mabadiliko wenye jamii kwa kuwa elimu ni njia pekee ya kuleta maendeleo kwa haraka katika ujenzi wa taifa . “Naupongeza uongozi wa shule kwa kuwekeza katika elimu na nawapongeza wazazi ambao wanawekeza katika elimu kwa kusomesha watoto wao maana elimu bora katika jamii inachangia kuleta mabadiliko ya nchi haraka”.Alisema
Mgeni rasmi akiangalia wanafunzi wakifanya majaribio ya sayansi.


Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Bw. Aloyce Siame, alisema kuwa katika kipindi cha miaka 10 tangu shule ianzishwe imeweza kushikilia rekodi ya kufanya vizuri kwa kufaulisha wanafunzi wa darasa la saba na la nne kwa kiwango cha juu na kuingia katika shule tano bora wilayani Ilala na shule bora 20 mkoani Dar es Salaam mfululizo hali ambayo imewajengea hari ya kuzidi kufanya vizuri kwa mwaka huu na miaka ijayo.



Hivyo makala SHULE YA GENIUS KINGS YAFANYA MAHAFALI YAKE YA 6 JIJINI DAR

yaani makala yote SHULE YA GENIUS KINGS YAFANYA MAHAFALI YAKE YA 6 JIJINI DAR Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SHULE YA GENIUS KINGS YAFANYA MAHAFALI YAKE YA 6 JIJINI DAR mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/08/shule-ya-genius-kings-yafanya-mahafali.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "SHULE YA GENIUS KINGS YAFANYA MAHAFALI YAKE YA 6 JIJINI DAR"

Post a Comment

Loading...