Loading...
title : Sudan yaalikwa mafunzo ya kijeshi.
link : Sudan yaalikwa mafunzo ya kijeshi.
Sudan yaalikwa mafunzo ya kijeshi.
MWAMBA WA HABARI
Khartoum
Nchi ya Sudan imepokea mualiko kutoka Marekani kuhusu kufanya mafunzo ya pamoja ya kijeshi na Misri, ukiwa ni mualiko wa kwanza wa aina hiyo kwa zaidi ya miongo mitatu.
Taarifa kutoka Mkuu wa jeshi la Sudan, Jenerali Emad al-Din Adawi amesema kuwa mualiko huo wa mazoezi ya pamoja yajulikanayo kama Bright Star yatakayofanyika nchini Misri.
Mkuu huyo wa jeshi la Sudan hivi karibuni wamefanya kikao na maafisa wa kijeshikutoka Marekani.
Amesema kuwa mkutano wao umefungua mlango kwa mazungumzo zaidi ambayo yanaweza kurejesha tena mahusiano kati ya Marekani na Sudan.
Mwezi Julai mwaka huu Marekani iliahirisha kwa miezi mitatu uamuzi wake wa kuiondolea vikwazo vya kiuchumi Sudan juu ya rekodi yake ya haki za binadamu na masuala mengine.
Uchumi wa Sudan umeporomoka tangu Sudan Kusini kujitenga mnamo mwaka 2011, na kuondoka na thuluthi tatu ya mafuta yanayozalishwa, ambacho ndio chanzo kikuu cha fedha za kigeni na mapato ya serikali yake.
Hivyo makala Sudan yaalikwa mafunzo ya kijeshi.
yaani makala yote Sudan yaalikwa mafunzo ya kijeshi. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Sudan yaalikwa mafunzo ya kijeshi. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/08/sudan-yaalikwa-mafunzo-ya-kijeshi.html
0 Response to "Sudan yaalikwa mafunzo ya kijeshi."
Post a Comment