Loading...
title : WANACHAMA wa Coastal Union ya Tanga waazimia kurudisha umoja kwenye klabu ili kuhakikisha timu hiyo inarejea Ligi Kuu Tanzania Bara.
link : WANACHAMA wa Coastal Union ya Tanga waazimia kurudisha umoja kwenye klabu ili kuhakikisha timu hiyo inarejea Ligi Kuu Tanzania Bara.
WANACHAMA wa Coastal Union ya Tanga waazimia kurudisha umoja kwenye klabu ili kuhakikisha timu hiyo inarejea Ligi Kuu Tanzania Bara.
WANACHAMA wa Coastal Union ya Tanga wameazimia kurudisha umoja kwenye klabu ili kuhakikisha timu hiyo inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza inarejea Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Akzungumza na mwandishi wetu baada ya kuisha mkutano wa wanachama kutoka Tanga, msemaji wa klabu hiyo maarufu Wagosi wa Kaya, Hafidh Kido alisema kwa mipango iliyokuwepo hakuna sababu ya kuifanya timu hiyo kongwe nchini kushindwa kurejea ligi kuu msimu ujao.
“Mkutano ulikuwa na ajenda nyingi lakini kubwa ilikuwa ni kuleta umoja na kubainisha mikakati ya kushiriki vema ligi daraja la kwanza msimu huu.
“Tumefanya usajili wa nguvu, wachezaji wengi waliokuwa wakishiriki ligi kuu msimu uliopita tumewanaka na tayari wamesharipoti kambini,” alisema Hafidh Kido na kuongeza:
“Hii ni Coastal Union mpya, wapenzi na wanachama wote uliokuwa ukiwajua wamerejea kwa ajili ya kuongeza nguvu. Sasa hivi Coastal Union ni wali ng’ombe hakuna njaa.”
Kwa upande wake Mwenyekiti Kamati ya Usajili na Mashindano, Hemed Hilal ‘Aurora’ alisema; “Makundi ndiyo yaliyoidhoofisha Coastal Union lakini leo nathibitisha wazi makund yamekufa na Coastal Union ni moja.”
Alisisitiza kuwa kila mmoja atimize wajibu wake ili msimu huu mambo yanyooke na Coastal Union irudi mahali panapostahili kwa sababu kushiriki ligi daraja la kwanza si hadhi yao.
Aidha mbali ya mambo mengine uongozi wa klabu hiyo ulitangaza jana kuwa kambi inaanza rasmi Jumatatu (leo) ambapo wachezaji wote waliosajili tayari wamesharipoti kambini.Kwa upande wake mchezaji wa zamani wa Coastal Union, Razak Yusuf 'Careca,' alisema Coastal ya mwaka huu ni moto wa kuotea mbali kinyume na watu wanavyoitazamia.
"Tayari tumeshapata nyumba ambayo wachezaji wote watakaa, tuna wachezaji wengi walioshiriki ligi kuu msimu uliopita ikiwemo Ndanda na African Lyon."Wapo wachezaji pia kama golikipa wa zamani wa Mtibwa na Simba, Hussein Shariff 'Casilas,' Baraka Jafari aliyekua kapteni African Lyon, mchezaji wa zamani wa Yanga, Athumani Idd 'Chuji,' Rashid Roshwa mfungaji bora wa Ndondo Cup iliyoisha hivi karibuni na mchezaji mkongwe Salvatory Ntebe," alisema Careca.
Aidha, mazoezi ya wachezaji yatafanyika asubuhi na jioni chini ya usimamizi wa Makocha Juma Mgunda na Joseph Lazaro. Asubihi yatafanyika katika uwanja mkongwe wa Mkwakwani na jioni yatafanyika katika uwanja wa Shule ya Sekondari Galanosi.
Coastal Union iliyoanzishwa mwaka 1948 ni miongoni mwa timu chache zilizoanzisha Ligi Kuu Tanzania Bara wakati huo ikiitwa Ligi ya Taifa na imejizolea sifa nyingi katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati kutokana na soka lililonyooka kaioka miaka ya 1960 hadi 1990.
Hivyo makala WANACHAMA wa Coastal Union ya Tanga waazimia kurudisha umoja kwenye klabu ili kuhakikisha timu hiyo inarejea Ligi Kuu Tanzania Bara.
yaani makala yote WANACHAMA wa Coastal Union ya Tanga waazimia kurudisha umoja kwenye klabu ili kuhakikisha timu hiyo inarejea Ligi Kuu Tanzania Bara. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WANACHAMA wa Coastal Union ya Tanga waazimia kurudisha umoja kwenye klabu ili kuhakikisha timu hiyo inarejea Ligi Kuu Tanzania Bara. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/08/wanachama-wa-coastal-union-ya-tanga.html
0 Response to "WANACHAMA wa Coastal Union ya Tanga waazimia kurudisha umoja kwenye klabu ili kuhakikisha timu hiyo inarejea Ligi Kuu Tanzania Bara."
Post a Comment