Loading...

MAYANGA ATAJA TAIFA STARS KUIVAA MALAWI

Loading...
MAYANGA ATAJA TAIFA STARS KUIVAA MALAWI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MAYANGA ATAJA TAIFA STARS KUIVAA MALAWI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MAYANGA ATAJA TAIFA STARS KUIVAA MALAWI
link : MAYANGA ATAJA TAIFA STARS KUIVAA MALAWI

soma pia


MAYANGA ATAJA TAIFA STARS KUIVAA MALAWI

Mwambawahabari

Kocha Mkuu wa timu ya Mpira wa Miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Salum Shabani Mayanga ametangaza kikosi kipya kitakachocheza na Malawi ‘The Flame’ katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa chini ya utaratibu wa kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
Wiki ya FIFA kwa mechi za kimataifa inatarajiwa kuanza Jumatatu Oktoba 2 hadi Jumatano ya Oktoba 11, mwaka huu ambako Tanzania imekubaliana kucheza Malawi kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam Jumamosi ya Oktoba 7, 2017 katika mchezo utakaoanza saa 10.00 jioni.
Katika kikosi hicho cha wachezaji 22, Kocha Mayanga ambaye aliteuliwa Januari 4, mwaka huu ameita nyota watano wanacheza soka nje ya mipaka ya Tanzania akiwamo nahodha wa kikosi hicho, Mbwana Ally Samatta.
Kikosi hicho kinachotarajiwa kuingia kambini Ijumaa Oktoba mosi, mwaka huu kwenye Hoteli ya Sea Scape iliyoko Kunduchi, Dar es Salaam kina makipa Aishi Manula (Simba SC), Ramadhani Kabwili (Young Africans) na Peter Manyika (Singida United).
Walinzi ni Gadiel Michael (Young Africans), Boniphas Maganga (Mbao FC), Abdi Banda (Baroka FC/Afrika Kusini), Kelvin Yondani (Young Africans), Salim Mbonde (Simba SC), Erasto Nyoni (Simba SC) na Adeyum Ahmed (Kagera Sugar).
Viungo wa kati ni Himid Mao – Nahodha Msaidizi (Azam FC), Hamis Abdallah (Sony Sugar/Kenya), Mzamiru Yassin (Simba SC) na Raphael Daud (Young Africans).
Viungo wa pembeni ni Saimon Msuva (Difaa El Jadidah/Morocco), Shizza Kichuya (Simba SC), Abdul Hilal (Tusker/Kenya), Ibrahim Ajib (Young Africans) na Morel Orgenes (FC Famalicao/Ureno).
Washambuliaji ni Mbwana Samatta (KRC Genk/Ubelgiji) na Mbaraka Yussuph (Azam FC). 
Benchi la Ufundi la Mayanga linaundwa na yeye mwenyewe ambaye ni Kocha Mkuu, Fulgence Novatus (Kocha Msaidizi), Ame Ninje (Kocha Msaidizi), Patrick Mwangata (Kocha wa Makipa), Danny Msangi (Meneja), Dkt. Richard Yomba (Daktari wa timu), Dkt. Gilbert Kigadye (Daktari wa Viungo) na Ally Ruvu (Mtunza Vifaa).


Hivyo makala MAYANGA ATAJA TAIFA STARS KUIVAA MALAWI

yaani makala yote MAYANGA ATAJA TAIFA STARS KUIVAA MALAWI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MAYANGA ATAJA TAIFA STARS KUIVAA MALAWI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/09/mayanga-ataja-taifa-stars-kuivaa-malawi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MAYANGA ATAJA TAIFA STARS KUIVAA MALAWI"

Post a Comment

Loading...