Loading...
title : MHASIBU MKUU WA WILAYA YA SIKONGE MATATANI KWA KUKALIA JARADA LA MTUMISHI TOKA MWEZI JULAI MWAKA HUU.
link : MHASIBU MKUU WA WILAYA YA SIKONGE MATATANI KWA KUKALIA JARADA LA MTUMISHI TOKA MWEZI JULAI MWAKA HUU.
MHASIBU MKUU WA WILAYA YA SIKONGE MATATANI KWA KUKALIA JARADA LA MTUMISHI TOKA MWEZI JULAI MWAKA HUU.
MwambawahabariNa Tiganya Vincent.
Sikonge
MHASIBU Mkuu (DT) wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge ameshitakiwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora kwa kukalia nyaraka za mstaafu kwa muda miezi zaidi ya miwili bila kushughulikia madai ya mtumishi huyo ya kulipwa kiunua mgongo.
Hali hiyo imetokea jana mjini Sikonge baada aliyekuwa Afisa Muuguzi Mkuu Paulo Madebe kudai kuwa tangu kumalizika kwa mkataba wake mwaka 2012 hadi leo hajalipwa kiinua mgongo chake licha ya taratibu mbalimbali kukamilika.
Madebe alisema kuwa alistaafu mwaka 2007 na baadaye alipata mkataba wa kuanzia mwaka 2010 hadi 2012.
Alisema kuwa baada ya kumalizika kwa mkataba wake amekuwa akifutilia fedha za kiinua mgongo na makato aliyokatwa kimakosa ya Mfuko wa PSPF bila mafanikio.
Madebe aliongeza kuwa baada ya kuona kuna ucheleweshaji kwa madai ya kukosekana kwa baadhi ya vielelezo aliamua kilifuatilia na kufanikiwa kuleta nyaraka katika Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge lakini wameshindwa kumalizia malipo yake.
Alisema kuwa pamoja na Mdhibiti naMkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kupitia madai na kutoa ushauri lakini DT amekataa kushighulikia Jarada lake ambapo aliongeza kuwa toka mwezi Julai liko mezani kwake.
Kufuatia hali hiyo Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amewapa siku mbili Mhasibu Mkuu wa Wilaya na Afisa Utumishi kuhakikisha jarida la mstaafu huyo linashughulikiwa na mhusika anajulisha ni lini atapata haki yake.
Alisema kuwa haiwezekani kila siku mzee kama yule anafutilia suala lake kwa zaidi ya miaka minne bila kupewa ufumbuzi na hivyo kujikuta akipoteza muda na fedha zake badala ya kupumzika.
Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Peres Magiri alishauri kuwa ipoa haja ya kuendesha zoezi la uhamisho wa ndani kwa watumishi wa Halmashauri ya Sikonge kwa kuwa wengi wao wamekaa eneo kwa muda mrefu na kujenga mazoea ambayo yamefanya kushindwa kuwajibika ipasavyo.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora baada ya kumaliza zoezi la kusikiliza kero za wakazi wa Sikonge anatarajia kuendelea na Wilaya nyingine.
Hivyo makala MHASIBU MKUU WA WILAYA YA SIKONGE MATATANI KWA KUKALIA JARADA LA MTUMISHI TOKA MWEZI JULAI MWAKA HUU.
yaani makala yote MHASIBU MKUU WA WILAYA YA SIKONGE MATATANI KWA KUKALIA JARADA LA MTUMISHI TOKA MWEZI JULAI MWAKA HUU. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MHASIBU MKUU WA WILAYA YA SIKONGE MATATANI KWA KUKALIA JARADA LA MTUMISHI TOKA MWEZI JULAI MWAKA HUU. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/09/mhasibu-mkuu-wa-wilaya-ya-sikonge.html
0 Response to "MHASIBU MKUU WA WILAYA YA SIKONGE MATATANI KWA KUKALIA JARADA LA MTUMISHI TOKA MWEZI JULAI MWAKA HUU."
Post a Comment