Loading...
title : Zahanati ya Vingunguti yafuzu na kupatiwa cheo cha nyota nne na serikali
link : Zahanati ya Vingunguti yafuzu na kupatiwa cheo cha nyota nne na serikali
Zahanati ya Vingunguti yafuzu na kupatiwa cheo cha nyota nne na serikali
Akizungumza mara baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Zahanati Ibrahim Aeshi Nduze, Naibu Meya Kumbilamoto ameeleza kuwa hali ya mara ya kwanza katika zahanati hiyo haikuwa shwari lakini kwa jitihada zake na kushirikiana na Halmashauri na Serikali alifanikiwa kufanya mambo mbalimbali katika maboresho ya zahanati hiyo na hatimae imefanikiwa kupewa hadhi ya nyota nne.
Akiyataja mambo waliyoyafanya katika Zahanati hiyo ni pamoja na Ununuzi wa Gari ya Wagonjwa (Ambulance), Mashine ya Kufulia,Jenereta, Choo kwa kinamama wanaojifungua, utanuzi wa maabara, ufungaji wa feni nne, mashne tatu za kupmia uzito kwa watoto,kipimo cha presha na kiti cha kubebea wagonjwa.
Zahanati nyingine zilizoweza kupandishwa hadhi Halmashauri ya Ilala ni pamoja na Zahanati ya Tabata, Mhongo la Ndege, Kinyerezi na Kadlugambwa.
Taarifa kutoka Kamati ya Zahanati imeeleza kuwa mwanzo zahanati yetu ilikua na nyota mbili ambapo hizo zahanati nyingine zilikua na nyota tatu hivyo vingunguti imepanda nyota mbili. Kamati hiyo imewashukuru wananchi kwa mawazo, maoni, na changamoto walizozitoa ambazo zimezifanyiwa kazi na ku pelekea zahanati hiyo kupata nyota mbili za ziada, kamati memshukuru pia Diwani Omary Said Kumbilamoto kwa kuwaongoza, kuwashauri, na kutoa mchango wa hali na mali ii kufikia malengo.
Hivyo makala Zahanati ya Vingunguti yafuzu na kupatiwa cheo cha nyota nne na serikali
yaani makala yote Zahanati ya Vingunguti yafuzu na kupatiwa cheo cha nyota nne na serikali Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Zahanati ya Vingunguti yafuzu na kupatiwa cheo cha nyota nne na serikali mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/09/zahanati-ya-vingunguti-yafuzu-na.html
0 Response to "Zahanati ya Vingunguti yafuzu na kupatiwa cheo cha nyota nne na serikali"
Post a Comment