Loading...
title : ATHMANI ANAWAOMBA MSAADA WATANZANIA
link : ATHMANI ANAWAOMBA MSAADA WATANZANIA
ATHMANI ANAWAOMBA MSAADA WATANZANIA
Na Yeremias Ngerangera, Namtumbo
Athmani Amani mkazi wa kijiji cha Naikesi kata ya kitanda wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma anawaomba watanzania kumsaidia fedha za kugharimia matibabu ya mtoto wake Shaziri Athmani (12) anayesumbuliwa na tatizo la moyo kuwa mkubwa.
Mtoto Shaziri Athamani ni mwanafunzi wa darasa la nne shule ya msingi Naikesi iliyopo kata ya Kitanda wilayani Namtumbo awali alikuwa anasumbuliwa na kuvimba miguu hali iliyokuwa inamkosesha masomo yake darasani mara kwa mara kuanzia mwaka 2016.
Mwaka huo huo mwezi Septemba baba yake alilazimika kumpeleka Hospitali ya Mkoa Songea kuangalia tatizo la kuvimba kwa miguu ya mtoto huyo na baada ya kupata vipimo wakashauriwa kuenda Hospitali ya Peramiho .
Bwana Athamani alidai kuwa hakuwa na fedha za kumpeleka mtoto peramiho kwa kipindi hicho na badala yake alirudi naye nyumbani Naikesi kwenda kuuza mifugo lakini fedha hizo hazikumwezesha kukidhi mahitaji ya kumtibu mwanoa katika Hospitali ya Peramiho baada ya kufika katika Hospitali hiyo na kumaliza fedha yake yote aliyokuwa nayo katika vipimo pekee .
Baada ya kupatiwa vipimo na kubaini Tatizo la mwanae alirudi na mwanae mpaka kijijini kwake kujipanga upya kwa ajili ya matibabu ya mwanae na kujitahidi kwa kile anachokipata anunue dawa kwa ajili ya mwanae huyo.
Hivyo makala ATHMANI ANAWAOMBA MSAADA WATANZANIA
yaani makala yote ATHMANI ANAWAOMBA MSAADA WATANZANIA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala ATHMANI ANAWAOMBA MSAADA WATANZANIA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/10/athmani-anawaomba-msaada-watanzania.html
0 Response to "ATHMANI ANAWAOMBA MSAADA WATANZANIA"
Post a Comment