Loading...
title : BENJAMIN SITA AKERWA NA UCHAFU, ASEMA SERIKALI INATUMIA FEDHA NYINGI KUTIBU MAGONJWA YANAYO SABABISHWA NA UCHAFU,ATOAAHADI KUCHIMBA KISIMA SHULE YA MSINGI MKWAWA.
link : BENJAMIN SITA AKERWA NA UCHAFU, ASEMA SERIKALI INATUMIA FEDHA NYINGI KUTIBU MAGONJWA YANAYO SABABISHWA NA UCHAFU,ATOAAHADI KUCHIMBA KISIMA SHULE YA MSINGI MKWAWA.
BENJAMIN SITA AKERWA NA UCHAFU, ASEMA SERIKALI INATUMIA FEDHA NYINGI KUTIBU MAGONJWA YANAYO SABABISHWA NA UCHAFU,ATOAAHADI KUCHIMBA KISIMA SHULE YA MSINGI MKWAWA.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya kinondoni Benjamini Sitta, akizungumza katika ufunguzi wa siku ya kunawa mikono Duniani iliyofanyika katika shule ya Msingi kigogo. (Picha zote na John Luhende mwambawahabari)
Baadhi ya wanafunzi wakitumbuiza mbele ya mgeni rasmi katika ufunguzi wa siku ya unawaji mikono
Baadhi ya waalimu wa shule ya msingi Kigogo, wakipokea zawadi ya sabuni ikiwa ni ishara ya ya kuhamasisha zaidi zoezi la usafi kwa wanafunzi shuleni hapo.
Baadhi ya wanafunzi wkimsikiliza mgeni Rasmi katika ufunguzi wa siku ya unawaji mikono
Baadhi ya waalimu wa shule ya msingi Kigogo, wakipokea zawadi ya sabuni ikiwa ni ishara ya ya kuhamasisha zaidi zoezi la usafi kwa wanafunzi shuleni hapo.
mwambawahabariMeya wa Manispaa ya Kinondoni Benjamini Sitta ametoa wito kwa watanzania wote kuzingatia umuhimu wa usafi hasa kwa kuzingatia zoezi la kunawa mikono kabla na baada ya kula au chochote kile ili kuweza kuepukana na baadhi ya magonjwa ambayo huwa ni rahisi kuepukika kwa urahisi.
Ameyasema hayo hivi leo wakati alipokuwa akifungua maadhimisho ya siku ya unawaji mikono Duniani maadhimisho ambayo yamefanyika katika shule ya msingi Kigogo iliyopo manispaa ya kinondoni Jijini Dar es salaam.
Aidha, ameongeza kuwa hivi sasa kumekuwa na ongezeko kubwa la baadhi ya magonjwa ambayo yanasababishwa na uchafu , magonjwa ambayo ni rahisi zaidi kuepukika kwa kuafuata kanuni za usafi,huku akibainisha kuwa wazazi/walezi husika ndio wanaopaswa kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha swala la afya kwa jamii,watoto,nyumba,au popote pale linazingatiwa na kuchukiliwa uzito kwani itasaidia pia katika kuondokana na baadhi ya magonjwa kama vile ya Kipindu pindu.
Sanjari na hayo meya Sitta amesema, baadhi ya watotozaidi ya milioni tatu na nusu hupoteza maisha kote duniani kwa kuugua Kipindu pindu huku watoto zaidi ya laki mbili katika jangwa la kusini mwa sahara hupoteza maisha huku katika manispaa ya kinondoni katika kipindi cha hadi mwaka jana watoto walioripotiwa ni sita ambao wote wameripotiwa kupoteza maisha kwa kuugua Kipindu pindu.
Ameongeza kuwa imewekwa siku hii muhimu ya Unawaji wa mikono ili kuimarisha na kuongeza ufanisi katika kutambua pamoja na kuelimisha zaidi baadhi ya matatizo ambayo huweza kusababishwa na kutozingatia usafi hasa wa kunawa mikono
Pamoja na hayo Mhe. Sitta katika hotuba yake ameahidi kuijengea kisima kimoja shule ya msingi mkwawa ilyopo kigogoo , ili kuwezesha kuchangia katika upatikanaji wa majisafi shuleni hapo ili kudumisha usafi na kuepukana na adha ya uchafu na changamoto za ukosefu wa maji zilizopo kwenye baadhi ya shule jambo ambalo hupelekea wanafunzi kuwawachafu hasamikono wanapotoka msalani.
Hivyo makala BENJAMIN SITA AKERWA NA UCHAFU, ASEMA SERIKALI INATUMIA FEDHA NYINGI KUTIBU MAGONJWA YANAYO SABABISHWA NA UCHAFU,ATOAAHADI KUCHIMBA KISIMA SHULE YA MSINGI MKWAWA.
yaani makala yote BENJAMIN SITA AKERWA NA UCHAFU, ASEMA SERIKALI INATUMIA FEDHA NYINGI KUTIBU MAGONJWA YANAYO SABABISHWA NA UCHAFU,ATOAAHADI KUCHIMBA KISIMA SHULE YA MSINGI MKWAWA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BENJAMIN SITA AKERWA NA UCHAFU, ASEMA SERIKALI INATUMIA FEDHA NYINGI KUTIBU MAGONJWA YANAYO SABABISHWA NA UCHAFU,ATOAAHADI KUCHIMBA KISIMA SHULE YA MSINGI MKWAWA. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/10/benjamin-sita-akerwa-na-uchafu-asema.html
0 Response to "BENJAMIN SITA AKERWA NA UCHAFU, ASEMA SERIKALI INATUMIA FEDHA NYINGI KUTIBU MAGONJWA YANAYO SABABISHWA NA UCHAFU,ATOAAHADI KUCHIMBA KISIMA SHULE YA MSINGI MKWAWA."
Post a Comment