Loading...

Taswa FC, Taswa Queens zazao zawadi zote za Tamasha la waandishi wa Habari la Arusha

Loading...
Taswa FC, Taswa Queens zazao zawadi zote za Tamasha la waandishi wa Habari la Arusha - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Taswa FC, Taswa Queens zazao zawadi zote za Tamasha la waandishi wa Habari la Arusha, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Taswa FC, Taswa Queens zazao zawadi zote za Tamasha la waandishi wa Habari la Arusha
link : Taswa FC, Taswa Queens zazao zawadi zote za Tamasha la waandishi wa Habari la Arusha

soma pia


Taswa FC, Taswa Queens zazao zawadi zote za Tamasha la waandishi wa Habari la Arusha

Katibu Mkuu wa Chama cha Waandishi wa habari wa mkoa wa Arusha, Mussa Juma (wa pili kulia) akikabidhi kombe la ushindi wa kwanza kwa nahodha wa Taswa FC, Wilbert Molandi mara baada ya kutwaa ubingwa kwa mara ya 12 mfululizo. anayeshuhudia ni mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto Omary.
Katibu Mkuu wa Chama cha Waandishi wa habari wa mkoa wa Arusha, Mussa Juma (wa pili kulia) akikabidhi kombe la ushindi wa kwanza kwa nahodha wa Taswa Queens, Zuhura Abdinoor mara baada ya kutwaa ubingwa kwa mara ya tano mfululizo. Wanaoshuhudia ni mratibu wa Taswa Queens, Sia Mafuwe, na Mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto Omary.
Wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Taswa SC wakiwa katika picha ya pamoja.

Arusha. Timu ya mpira wa miguu ya waandishi wa habari za michezo nchini (Taswa FC) nay a mpira wa pete (Taswa Queens) zimetwaa ubingwa wa tamasha la 13 la vyombo vya habari la Arusha (Arusha Media Bonaza) lililofanyika kwenye viwanja vya General Tyre.

Wakati Taswa FC ikitwaa nafasi ya kwanza kwa mpira wa miguu baada ya kujikusanyia pointi saba, Taswa Queens ilitwaa nafasi ya kwanza kwa upande wa netiboli baada ya kuifunga Taswa Arusha kwa mabao 19-7 katika mchezo wa kusisimua ulioshuhudiwa na Mkuu wa Mkoa wa  Arusha, Mrisho Gambo.

Mbali ya kutwaa vikombe vya mpira wa miguu, timu hizo ambazo zinadhaminiwa na kampuni ya MultiChoice Tanzania (DSTV), benki ya TPB na Property International Limited, pia ilihakikisha vyombo vya ha ari vya Arusha vinaondoka  mikono mitupu baada ya kutwaa nafasi ya kwanza katika mbio za kufukuza kuku. Magret Elia ambaye ashinda kuku wawili na Veronica Deus aliyeshinda mara moja.

Taswa FC ilianza kampeni yake kutetea ubingwa wake kwa kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Radio Sun Rise. Timu hiyo ilisawazisha kupitia kwa Zahoro Mlanzi  baada ya gonga safi za  Wilbert Molandi, Ali Salum na Saidi Seif.
Taswa FC ilibadili upepo wa mashindano hayo baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Taswa Arusha baada ya Ibrahim “Maestro” Masoud kufunga kwa penati na Nicholas Ndifwa kufunga la pili baada ya ushirikiano mzuri wa Martin Shilla, Edward Mbaga, Kulwa Ndege na Muhidin Sufiani.

Mchezo wa kuamua nani bingwa ulikuwa kati ya Taswa SC dhidi ya Radio 5 ambapo Saidi Seif alifunga bao la ushindi kufuatia pasi ya Mohamed Akida aliyecheza vizuri na Majuto Omary.
Timu ya netiboli, Taswa Queens ilishinda mchezo wa fainali kwa mabao 19-7, mchezo ambao ulihudhuliwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.

Taswa Arusha iliongoza dakika za mwanzoni mwa mchezo kabla ya Taswa Queens kubadili kibao na kuongoza kwa 10-5 mpaka mapumziko. Sharifa Mustafa, Veronica Deus na  Imani Makongoro walifunga kwa  Taswa Queens ambapo Zuhura Abduknoor, Magreth, Elia, Elizabeth Mbassa,  Amina Abdallah, Rukia Juma, Dosca Munthali alihakikisha Taswa Arusha ambayo ilikuwa chini ya  Rehema Mussa haifurukuti.

Kwa matokeo hayo, Taswa  SC zilitwaa kombe na fedha taslimu Sh 300,000. Mwenyekiti wa timu hiyo, Majuto Omary aliwapongeza wachezaji wake na wadhamini, Benki ya TPB, DSTV na Property International Limited kwa kufanikisha safari hiyo.

Katibu Mkuu wa Taswa Arusha, Mussa Juma alizipongeza timu zote kwa kushiriki katika bonanza hilo ambalo lilidhaminiwa na  Hifadhi za Taifa (TANAPA) Mifuko ya hifadhi ya Jamii ya LAPF na PSPF, Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro,  Coca Cola, kampuni ya ya vinywaji baridi ya SBC (T) Limited na Palace Hoteli.


Hivyo makala Taswa FC, Taswa Queens zazao zawadi zote za Tamasha la waandishi wa Habari la Arusha

yaani makala yote Taswa FC, Taswa Queens zazao zawadi zote za Tamasha la waandishi wa Habari la Arusha Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Taswa FC, Taswa Queens zazao zawadi zote za Tamasha la waandishi wa Habari la Arusha mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/10/taswa-fc-taswa-queens-zazao-zawadi-zote.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Taswa FC, Taswa Queens zazao zawadi zote za Tamasha la waandishi wa Habari la Arusha"

Post a Comment

Loading...