Loading...
title : USAJILI VITAMBULISHO VYA TAIFA WAENDELEA MKOA WA GEITA
link : USAJILI VITAMBULISHO VYA TAIFA WAENDELEA MKOA WA GEITA
USAJILI VITAMBULISHO VYA TAIFA WAENDELEA MKOA WA GEITA
Wananchi wa Halmashauri ya mji Geita, mkoani Geita wameendelea kujitokeza kwa wingi kushiriki katika zoezi la usajili na utambuzi linaloendeshwa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa. Zoezi hili ambalo kwa sasa linaendelea mikoa yote ya Kanda ya Ziwa na Kaskazini limekuwa ni fursa nzuri na muhimu kwa wananchi kusajiliwa na kuwezeshwa kushiriki katika shughuli za maendeleo kutokana na umuhimu wa taarifa zinazokusanywa.
Pindi mfumo huu utakapokamilika wananchi watawezeshwa kupata huduma mbalimbali kwa urahisi pamoja na kusaidia Serikali kuimarisha Ulinzi na Usalama wa nchi kwani Kitambulisho hiki kitakuwa ufunguo kwa mifumo mingine ya Serikali kubadilishana taarifa.
Wananchi wa mtaa wa Station kata ya Mtakuja Halmashauri ya Mji Geita katika foleni wakisubiri kusajiliwa Vitambulisho vya Taifa, wakati wa zoezi la usajili linaloendelea mkoani humo.
Wananchi kata ya Bulela Halmashauri ya Mji Geita wakisubiri huduma ya usajili wakati wa zoezi la usajili wa Vitambulisho vya Taifa linaloendelea Mkoani Geita.
Wananchi kata ya Bulela Halmashauri ya Mji Geita wakisubiri huduma ya usajili wakati wa zoezi la usajili wa Vitambulisho vya Taifa linaloendelea Mkoani Geita.
Afisa Msajili Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, akiendelea na zoezi la usajili Vitambulisho vya Taifa kwa Wananchi wa mtaa wa Station kata ya Mtakuja Halmashauri ya Mji Geita.
Maafisa wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa wakiendelea na zoezi la uingizaji wa taarifa za wananchi katika zoezi la usajili Vitambulisho vya Taifa linaloendelea katika Halmashauri ya Mji Geita Mkoani Geita.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uratibu Ofisi za wilaya Bi. Rehema Kionaumela akitoa maelekeza kwa Maafisa wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Mkoani Geita kuhusu taratibu mbalimbali wakati wa maandalizi ya zoezi la usajili wa Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi wa Halmashauri ya Mji Geita.
Hivyo makala USAJILI VITAMBULISHO VYA TAIFA WAENDELEA MKOA WA GEITA
yaani makala yote USAJILI VITAMBULISHO VYA TAIFA WAENDELEA MKOA WA GEITA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala USAJILI VITAMBULISHO VYA TAIFA WAENDELEA MKOA WA GEITA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/10/usajili-vitambulisho-vya-taifa.html
0 Response to "USAJILI VITAMBULISHO VYA TAIFA WAENDELEA MKOA WA GEITA"
Post a Comment