Loading...
title : SERIKALI, MADHEHEBU YA DINI KUENDELEZA USHIRIKIANO
link : SERIKALI, MADHEHEBU YA DINI KUENDELEZA USHIRIKIANO
SERIKALI, MADHEHEBU YA DINI KUENDELEZA USHIRIKIANO
NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA
SERIKALI itaendeleza ushirikiano na madhehebu yote ya dini kwa kuwa ndiyo msingi wa amani na utulivu uliopo nchini na kuwataka viongozi wa dini waisaidie kufichua ubadhirifu wa mapato ya serikali na kuiwezesha kuleta maendeleo ya nchi kwa maslahi ya wananchi. Kauli hiyo ilitolewa juzi na Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Dk. Severin Mathias Lalika kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela,kwenye kongamano la maadhimisho ya miaka 50 ya Baraza Kuu la WaislamuTanzania (BAKWATA) yaliyofanyika kimkoa jijini humu.
“Tunaamini madhehebu ya dini ni msingi wa amani na utulivu wa nchi yetu, hivyo tutaendelea kushirikiana kwa sababu viongozi wa kiroho mmeshikilia roho zetu hata mkitangulia kusema jambo letu la serikali linakubalika kwa haraka kwenye jamii,”alisema Mongela. Alisema Yesu na Mtume Muhhamad hakuna mahali hawakuhubiri upendo kwa matendo, amani na utulivu ambavyo kuwepo kwake ndio maendeleo na kutoa wito kwa viongozi wa dini waendelee kuisaidia serikali kuhubiri amani kwenye nyumba za ibada kwani hata katiba na sheria zilizotungwa msingi wake ni vitabu vya dini.
Alieleza kuwa taasisi mbalimbali za dini kushirikiana kuadhimisha miaka 50 ya BAKWATA mkoani Mwanza iwe chachu ya kupiga vita ya kiimani kati ya madhehebu ya Kiislamu na Kikrito ikizingatiwa ni watoto wa baba mmoja (Ibrahim), hivyo wakielewa hilo hakuna sababu ya kukosana. Mongela alisema serikali haijawahi kuwa na nia mbaya na wananchi wake lakini zipo changamoto zinazokwamisha maendeleo nazo ni dawa za kulevya, mimba za utotoni na VVU, hivyo viongozi wa dini shughuli zao za kiroho wanazofanya wayahubiri hayo.

Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Mwanza Alhaji Sheikh Hasani Musa Kabeke akizungumza na waumini wa dini ya Kiislamu wakati wa kuchangia damu kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya BAKWATA yaliyofanyika kimkoa jijini Mwanza.
Mgeni rasmi wa zoezi la kuchangia damu kwa waumini wa dini ya kiislamu jijini Mwanza, Mratibu wa Mabalozi wa Usalama Barabarani Kanda ya Ziwa Abel Ntahorutoba akizungumza kwenye zoezi hilo wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya BAKWATA.
Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Mwanza na Mratibu wa Mabalozi wa Usalama Barabarani Abel Ntahorutoba (kushoto) wakichangia damu kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza, Sekou Toure.
Katibu Muhtasi wa BAKWATA Mkoa wa Mwanza aliyehamika kwa jina moja la Sikitu akichangia damu siku ya maadhimisho ya miaka 50 ya BAKWATA mkoani hapa. Wa kwanza kulia ni Katibu wa JUWAKITA Dotto Mangu.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya BAKWATA Mkoa wa Mwanza Nurdin Mbaji akisiriki kuchagia damu kwenye maaadhimish ya miaka 50 ya baraza hilo.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala SERIKALI, MADHEHEBU YA DINI KUENDELEZA USHIRIKIANO
yaani makala yote SERIKALI, MADHEHEBU YA DINI KUENDELEZA USHIRIKIANO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI, MADHEHEBU YA DINI KUENDELEZA USHIRIKIANO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/serikali-madhehebu-ya-dini-kuendeleza.html
0 Response to "SERIKALI, MADHEHEBU YA DINI KUENDELEZA USHIRIKIANO"
Post a Comment