Loading...

VIJANA WASHAURIWA KUWATUNZA WAZEE

Loading...
VIJANA WASHAURIWA KUWATUNZA WAZEE - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa VIJANA WASHAURIWA KUWATUNZA WAZEE, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : VIJANA WASHAURIWA KUWATUNZA WAZEE
link : VIJANA WASHAURIWA KUWATUNZA WAZEE

soma pia


VIJANA WASHAURIWA KUWATUNZA WAZEE


Na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW

Vijana nchini wameshauriwa kujitolea na kuwatunza wazee katika maeneo yao ili kupata ushauri na busara za wazee hao kwa maendeleo yao na taifa.

Hayo yamesemwa Mjini Dodoma na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Alhaji Ali Hassan Mwinyi alipokuwa akizungumza na wazee katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani yanayofanyika kila Oktoba Mosi ya kila mwaka. Mhe. Mwinyi amesema kuwa jukumu la kuwatunza na kuwalea wazee sio la Serikali pekee bali jamii pia ina nafasi yake katika kuwatunza wazee hasa Vijana.

Mhe. Mwinyi ameongeza kuwa Serikali imejitaidi sana kuweka mazingira mazuri kwa wazee kwa kuwapatia huduma za Afya na kuwatunza wazee wote ambao hawana ndugu wa kuwatunza katika makambi mbalimbali ya wazee nchini. “Niwaombe vijana mtutunze sisi wazee kwani na sisi tulikuwa vijana kama ninyi na mkiweka utamaduni huu utawasaidia na ninyi mkiwa wazee hapo baadae” alisema Mhe. Mwinyi.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi akitoa zawadi kwa mmoja wa wazee wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma Oktoba 01,2017. 
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi akiangalia moja ya bidhaa zinazozalishwa na wazee katika moja ya banda la Maonesho wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma Oktoba 01,2017.Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW .



Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi akiwapungia mkono wazee wakati wakiingia kwa maandamano kuadhimisha Siku ya Wazee Duniani iliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma Oktoba 01,2017.


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana akitoa salamu za Mkoa kwa Mgeni Rasmi wa Siku ya Wazee Duniani Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma Oktoba 01,2017. 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akitoa maelezo kuhusu utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Wazee ya Mwaka 2003 kwa Mgeni wa Siku ya Wazee Duniani Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma Oktoba 01,2017. 



Hivyo makala VIJANA WASHAURIWA KUWATUNZA WAZEE

yaani makala yote VIJANA WASHAURIWA KUWATUNZA WAZEE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala VIJANA WASHAURIWA KUWATUNZA WAZEE mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/10/vijana-washauriwa-kuwatunza-wazee.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "VIJANA WASHAURIWA KUWATUNZA WAZEE"

Post a Comment

Loading...